TANGAZO


Friday, December 28, 2012

TASWA FC yakubali kichapo cha mabao 4-0 Bagamoyo mbele ya Veterani wa mji huo wa Kihistoria

 

 
Kikosi cha timu ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA FC), kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo wa kirafiki kati timu hiyo na Bagamoyo Veteran, mchezo uliofanyika uwanja wa Mawanakerenge, mjini Bagamoyo jioni ya leo, ambapo timu ya TASWA FC, imekubali kichapo cha mabao 4-0, mbele ya  maveterani hao, wa mji wa Kihistoria Bagamoyo Veteran. Timu ya TASWA FC, imeshiriki katika mchezo huo, ikiwa ni moja ya programu ya mkutano wa chama hicho, unaotarajiwa kufanyika kesho, Hoteli ya Kiromo View, mjini Bagamoyo, ambapo utafunguliwa na Ridhiwani Kikwete na Kufungwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Assah Mwambene.
 
 
Kikosi cha timu ya Bagamoyo Veteran, kilichotoa kichapo cha mabao 4-0 kwa timu ya TASWA FC mjini Bagamoyo, kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo huo mjini humo leo.
 
 
Baadhi ya waandishi wa habari za michezo, ambao ni mashabiki wa timu hiyo, wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
 
 
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Klabu ya Simba, Ibrahim Masoud 'Maestro' (katikati), akizungumza na Mzee Willy Chiwango wa gazeti la This Day (kulia) na Beny Kisaka, Mkurugenzi Mwanadamizi Gazeti la Jambo Leo.
 
 
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed Kipozi (wa pili kulia), akizungumza na mwandishi mkongwe kutoka Zanzibar, Said Salim Salim, huku wanahabari wengine wakifuatilia mazungumzo hayo.
 
 
Mchezaji wa timu ya TASWA FC na Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto, akimiliki mpira mbele ya beki wa timu ya Bagamoyo Veterani katika mchezo huo, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mwanakerenge, mjini Bagamoyo leo.
 
 
Mchezaji wa timu ya TASWA FC, Shafii Dauda, akimiliki mpira huku beki wa timu ya Bagamoyo Veterani akiuwania kutaka kuuchukua. Katikati ni mchezji wa timu ya TASWA FC, Mohamed Akida.
 
 
Mshauri wa timu ya TASWA FC, Masoud Sanani, akihimiza wachezaji hiyo, kucheza kwa bidii baada ya kuchapwa magoli 4-0, huku wachezaji wa timu hiyo, wakishangaa wasijue la kufanya wakati zikiwa zimesalia dakika chache za majeruhi. (Picha zote na John Bukuku wa Fullshangwe)

No comments:

Post a Comment