Msanii wa kike anaechipukia na kung"ara katika fani ya muziki nchini Tanzania, Mwanaisha Nyange 'Dyana', akiongea na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, alipokuwa, alipokuwa akitoa shukranii zake kwa Aljazerra Entertaiment kwa kumsaidia kumtoa msanii huyo kimuziki, bila ya kuwasahau, wadau mbalimbali wote wa muziki nchini ambao amesema ndio waliomsaidia kumfikisha hapo alipo sasa katika sanaa hii ya muziki huu wa kizazi kipya , kwani bila ya kupata ushirikiano wao asingeweza kufikia hapa alipo. . (kushoto) ni Msemaji wa Aljazerra Entertaiment Simon John
Msanii Richard Lusinga 'Richie Mavoko', akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akiwashukuru waandishi wa habari, wapenzi na wadau wa muziki nchini, kwa kumuunga mkono hadi kufika mafanikio aliyonayo. Kushoto ni msanii Mwanaisha Nyange 'DYANA'. (Picha zote na Mwanakombo Jumaa - MAELEZO)
Msanii Richie Mavoko (kulia), pamoja na msanii Mwanaisha Nyange (kushoto) 'DYANA' wakionesha manjonjo yao, mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani), leo jijini Dar es Salaam wakati wakitoa shukrani kwa wadau wa muziki nchini kwaniaba ya Kampuni ya Aljazerra Entertaiment ambayo ilianza kazi zake 01-04-2004 za kuwa saidia wasanii mbalimbali wenye vipaji vya kuimba, kucheza na maagizo. Hadi sasa imefanikiwa kumtoa kisanii, Diamond Plutim, Sam wa Ukweli, Dyana, na Richie Mavoko na wengine wengi.
Msanii Richie Mavoko (katikati), akiimba moja ya wimbo wake, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuwashukuru pamoja na wadau wa muziki huo nchini. Kushoto ni msanii Mwanaisha Nyange.
No comments:
Post a Comment