TANGAZO


Saturday, December 29, 2012

Ridhiwani Kikwete afungua Mkutano Mkuu wa TASWA Bagamoyo


Mwenyekiti wa Kamati ya Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana, Ridhiwani Kikwete, akihutubia alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) leo, Hoteli ya Kiromo, Bagamoyo, mkoani Pwani. (Picha zote na Richard Mwaikenda)
Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto akizungumza muda mfupi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Ridhiwani Kikwete kufungua mkutano huo.
Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando akitangaza ajenda za mkutano huo. Kulia ni Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto na mgeni rasmi Ridhiwani Kikwete.
Mgeni rasmi Ridhiwani Kikwete (kulia), akiwa na Mweyekiti wa TASWA, Juma Pinto, alipowasili Hoteli ya Kiromo, Bagamoyo kuufungua mkutano huo.
Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto na mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano wa chama hicho, Ridhiwani wakibadilishana mawazo.
Baadhi ya waandishi wa habari, ambao ni wajumbe wa mkutano huo wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakitendeka kwenye mkutano huo. Jumla ya wanachama 107, walishiriki kwenye mkutano huo.
Wanachama Somoe Ng'itu (kushoto), Anjela Msangi na Tom Chilala wakishiriki kwenye mkutano huo.
Baadhi ya wanachama wakishiriki kuomba dua, iliyoombwa kabla ya kuanza mkutano huo.
 Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto (kulia), akizungumza  wakati wa ufunguzi wa mkutano huo. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wake, Amir Mhando na mgeni rasmi katika ufunguzi huo, Ridhiwani Kikwete.
Mjumbe wa mkutano huo, Rajab Mhamila akijitambulisha kwa mgeni rasmi.
Katibu Mkuu wa zamani wa TASWA, Mwina Kaduguda akijitambulisha kwenye mkutano huo.
Mwandishi wa habari mkongwe wa habari za michezo nchini, Willy Chiwango, akijitambulisha katika mkutano huo.
 Sehemu ya wajumbe wa mkutano huo, wakisikiliza maelezo mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa.
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TASWA, wakimsikiliza mgeni rasmi, Ridhiwani Kikwete, wakati alipokuwa akiufungua mkutano huo.
Baadhi ya waandishi wakiwa kwenye mkutano huo.
Mgeni rasmi kwenye mkutano huo, Ridhiwani Kikwete (katikati), akipongezwa na Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando (kushoto), pamoja na Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto baada ya kuufungua mkutano huo.
Ofisa Ushirika wa Wilaya ya Ilala, Francis Lwambano akitoa mada ya uanzishwaji wa Saccos na faida zake kwa wanachama.
Wanachama wa TASWA, wakisikiliza maelezo mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.

No comments:

Post a Comment