Wafanyakazi wa mgodi Afrika Kusini wakigoma
Mkurugenzi mkuu wa kiwanda cha kuchimba madini ya platinum ya
Lonmin amejiuzulu, miezi minne baada ya mgomo wa wafanyakazi katika mgodi wake
wa Marikani nchini Afrika Kusini, iliyosababisha vifo vya watu 44.
Ian Farmer hajakuwa ofisini tangu mwezi Agosti baada ya kulazwa
hospitalini.
Afisa mkuu anayesimamia masuala ya ya fedha Simon Scott, ataendelea kuhudumu
kama kaimu afisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo, hadi mridhi wa Bwana Farmers,
atakapoteuliwa.
Kampuni hiyo ambayo imeorodheshwa kwenye masoko ya hisa ya Johannesburg na London, ililazimika kuomba fedha zaidi dola milioni 817 kutoka kwa wenye hisa wake, ili ilishindwe kulipa madeni yake na kukiuka sheria na masharti ya mikopo.
Tarehe kumi na sita mwezi wa nane mwaka huu wafanyakazi 34 wa kampuni hiyo walipigwa risasi na polisi, tukio ambalo lilitajwa kuwa mbaya zaidi tangu kumalizika kwa utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini mwaka wa 1994.
Wengine kumi, wakiwemo maaafisa wawili wa polisi waliaga dunia katika maandamano hayo ya wafanyaakazi wa migodi.
No comments:
Post a Comment