Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge
wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa (wa pili kushoto) akijumuika pamoja na
Baadhi ya Wabunge wanaounda timu ya Bunge Sports inayoundwa na wabunge kutoka
Baraza la Wawakilishi na Bunge la Jamhuri,wakati wa Chakula cha Mchana
alichowaandalia Nyumbani kwake, Ngarashi Wilayani Monduli jana.Wengine pichani
kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo, Amos
Makalla, Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Iddi Azzan pamoja na Mwenyekiti wa CCM,
Wilaya ya Monduli, Reuben ole Kunai.
Baadhi ya Wabunge na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakiwa katika hafla ya chakula cha mchana nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa, Monduli.
Baadhi ya Wabunge na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakipata chakula cha mchana nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa, Monduli.
Wabunge wanaounda timu ya
Bunge Sports inayoundwa na wabunge kutoka Baraza la Wawakilishi na Bunge la
Jamhuri wakipata Chakula cha Mchana kilichoandaliwa na Waziri Mkuu Mstaafu na
Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa Nyumbani kwake,Ngarashi Wilayani
Monduli jana.Mh. Lowassa alikutana na Wabunge hao ili kujadili maswala mbali
mbali yahusuyo Michezo hapa nchin,wakati timu hiyo ikiwa kambini jijini
Arusha, kujiandaa kwenda jijini Nairobi kwenye Mashindano ya Afrika
Mashariki.
WAZIRI Mkuu Mstaafu na Mbunge
wa Monduli Mh. Edward Lowassa amewashauri wabunge wa timu ya Bunge Sports
kufikiri juu ya kutunga sera ya michezo itakayoruhusu kuanzishwa kwa Shule za
Michezo (Sports Academy) hapa nchini.
Lowassa ameyasema hayo
jana,baada ya kuialika nyumbani kwake timu hiyo iliyopiga kambi ya jijini Arusha
tayari kwa mashindano ya Mabunge ya Afrika Mashariki jijini
Nairobi.
“Nilisikitika kweli Timu ya
Taifa ya Kilimanjaro Stars ilipofungwa na Burundi kwenye mchezo wa pili wa
Mashindano ya CECAFA huni Uganda, pamoja na juhudi za Rais Jakaya Kikwete kuleta
makocha bado tumefungwa na Burundi iliyotoka kwenye vita juzi!.
“Nyinyi ni watunga Sera, ni
wachezaji mnajua changamoto zinazofanya tusifike juu, umefika wakati wa kuwa na
Shule za Michezo zinazotambuliwa na Sera zetu.
“Mpira ni chakula cha
Watanzania, wanapenda mpira sana. Napendekeza baada ya kurejea anzeni kufikiria
juu ya kutunga Sera ya kuwa na Shule za Michezo. Kipingu amejitahidi kuwa na
kitu kama hiki lakini amebakia peke yake hakuna anayemuunga mkono,” alisema
Lowassa.
Alisema kuwapo kwa Timu ya
Bunge Sports kutasaidia kufikiria juu ya mafanikio ya mchezo wa mpira wa miguu,
pete na michezo mingine.
Kwa upande wake Naibu Waziri
wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh. Amos Makalla aliyeongozana na timu
hiyo alimwambia Mh. Lowassa kwamba serikali ipo katika hatua za mwisho za
kukamilisha Sera za michezo.
“Sera na sheria za sasa za
michezo kweli haziendani kabisa na wakat,zote ni za zamani. Serikali imejipanga
kuzifanyia kazi.
“Changamoto uliyoitoa ya
kuanzisha Shule za Michezo na kuendeleza michezo nchini tunaipokea na
tutaifanyia kazi.
“Nilipoteuliwa kuwa Naibu
Waziri kwenye Wizara hii niliwaambia watu na binafsi namshukuru Rais Kikwete,
kwamba upele ulipata mkunaji kwani mimi ni mwanamichezo na uwanjani ni kiungo
mchezeshaji,” alisema Makala.
Naye Mwenyekiti wa Timu hiyo
ya Bunge Sports inayoundwa na wabunge kutoka Baraza la Wawakilishi na Bunge la
Jamhuri, Iddi Azan alimshukuru Mh. Lowassa kwa mawazo yake na kuahidi kuyafanyia
kazi.
“Kwanza tunaahidi ushindi kwa
nchi, Bunge letu na haya uliyoyasema tunaahidi kuendelea kuyafanyia kazi kwani
tunatambua sheria na Sera za michezo zimepitwa na wakati,” alisema
Azan.
Timu hiyo ya Bunge Sports
ilikuwa na wachezaji wake wote waliopo kwenye kambi jijini Arusha wanaounda timu
ya Mpira wa miguu na Pete.
No comments:
Post a Comment