Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya, akikabidhi zawadi za Sikukuu ya Krismas na Mwaka mpya wa 2013 kwa Yatima wa kituo cha Bethania, mjini Sumbawanga. Katika msimu huu wa Sikukuu, Mkuu huyo wa Mkoa ameamua kusherehekea kwa kuwatembelea yatima, wafungwa na mahabusu wa gereza la Sumbawanga na gereza la Mollo kwa kuwapa chakula cha sikukuu pamoja na kusikiliza kero zao mbalimbali. Zawadi alizotoa ni mbuzi, mchele pamoja na sabuni za kufulia kwa watoto yatima wa kituo cha Bethania, vyote vikiwa na thamani ya sh. 380,000/=
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Injinia Stella Manyanya akiwa kwenye picha ya pamoja na Yatima wa kituo cha Bethania cha mjini Sumbawanga waliofaulu na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2013 katika shule mbalimbali mkoani Rukwa. Mkuu huyo wa Mkoa ameahidi kugharamia masomo yao kwa kidato cha kwanza na sare za shule pamoja na vitendea kazi vingine. Kulia ni Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Sumbawanga, Festo Chonya akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo, Methew Sedoyyeka.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Injinia Stella Manyanya akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Yatima wa kituo cha Bethania, mjini Sumbawanga alipowatembelea kwa ajili ya kuwafariji kwa chakula katika msimu huu wa sikukuu ya Krismas na Mwaka mpya.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Injinia Stella Manyanya, akizungumza na Yatima wa kituo cha Bethania. Kulia ni Mkuu wa kituo hicho, Emmanuel Mwampimbwe. Mkuu huyo wa Mkoa aliagiza watoto yatima katika kituo hicho, pamoja na vituo vingine watambuliwe na watengenezewe vitambulisho vitakavyowawezesha kupatiwa huduma bure katika hospitali za Serikali mkoani Rukwa.
ASP. A. Kimati, akisoma taarifa ya gereza la Mollo kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Injinia Stella Manyanya alipotembelea gereza hilo jana, kutoa salamu na chakula cha sikukuu kwa wafugwa wa gereza hilo na kuskiliza kero zao mbalimbali. Mkuu huyo wa Mkoa alipokea kero mbalimbali kutoka kwa wafugwa 195 wa gereza hilo, ikiwemo uhaba wa sare za wafungwa, wafugwa kutopewa nakala za hukumu zao, kesi zao kusikilizwa kwa Kiswahili lakini hukumu kuandikwa Kiingereza, kutokukubalika kwa dhamana zao, kutokuwepo kwa hakimu katika Wilaya ya Nkasi na baadhi ya kesi kuchelewa kuskilizwa.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Injinia Stella Manyanya, akitoa majumuisho ya ziara yake gerezani Mollo kwa kuzungumza na viongozi wa Jeshi la Polisi na la Magereza mkoani humo, ambapo aliahidi kufuatilia kero zote zilizowasilishwa kwa kushirikiana na pande zinazohusika kuhakikisha zinapatiwa ufumbuzi. Alisema kuwa ataendelea kuweka msukumo wa ujenzi wa Mahakama za Nkasi na Wilaya mpya ya Kalambo. Aidha aliutaka uongozi wa gereza hilo, kufyatua matofali kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya wafungwa katika gereza hilo, ambapo yeye atasaidia upatikanaji wa mabati na vifaa vingine vya madukani, kwa sasa mabweni yanayotumika katika gereza hilo ni ya mabati magumu ambayo kutokana na hali ya hewa ya maeneo hayo, huwa na baridi kali wakati wa msimu wa baridi. (Picha na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)
No comments:
Post a Comment