TANGAZO


Wednesday, December 26, 2012

Matukio mbalimbali ya Ibada ya Krismas jijini Dar es Salaam leo

Askofu Msaidi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa (katikati), akiongoza Ibada ya mkesha wa Sikuu ya Krismasi katika Kanisa la Mtakatifu Petro, Oysterbay jijini Dar es Salaam juzi. Kushoto ni Paroko wa kanisa hilo, Padri Joseph Mosha. 
 
 
 
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa, akitoa mahubiri wakati wa ibada ya Krismasi, jijini Dar es Salaam leo.
 
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa, akitoa baraka kwa waumini wa Usharika wa Azania Front baada ya ibada ya Krismasi jijini leo.
 
Mmiliki wa Mtandao wa Kijamii wa www.mwaibale.blogspot.com, Dotto Mwaibale akipeana mkono na Askofu Mkuu wa KKKT, Dk. Alex Malasusa baada ya ibada ya Krismasi iliyofanyika leo, katika Usharika wa Azania Front. Kulia ni mmiliki wa mtandao wa Mzuka wa Fungo, Omary Fungo.
 
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa, akiwa amembeba mtoto, Prisca John Mkony. Kushoto ni Sia Robinson na Jane Mkony akiwa amembeba mtoto, Patricia.
 
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa, akiwa amembeba mtoto, Prisca John Mkony.
 
Baadhi ya waumini wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph, wakiwa katika ibada ya Sikukuu ya Krismas.
Mkurugenzi wa Free Media Ltd, Liliani Mtei (kulia), akiwa na baadhi ya waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), wakisikiliza mahubiri yaliyokuwa yakitolewa na Askofu wa kanisa hilo, Dk. Alex Malasusa (hayupo pichani), wakati wa ibada ya Krismasi.
 
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa akipeana mkono na muumini wa kanisa hilo, Sevestine Mtunga baada ya ibada ya Sikukuu ya Krismasi iliyofanyika katika kanisa la Azania Front jijini Dar es Salaam.
 
Baadhi ya akinamama waliojifungua wakati wa mkesha wa Sikukuu ya Krismasi wakiwa na watoto wao katika hospitali ya Mwananyamala, jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Fatuma Shaban mkazi wa Vingunguti, Lucy Dominick mkazi wa Mwananyamala na Moshi Mengi, mkazi wa Manzese.
 
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa akitoa Baraka kwa mtoto, Patricia John Mkony mara baada ya ibada ya Sikukuu ya Krisimasi iliyofanyika katika kanisa la Azania Front, jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni, Rubani Mkuu mstaafu wa Serikali, Kapteni John Mkony, Jane John na Sia Robinson.
 
 
 
 
 
Sehemu ya waumini wa Kanisa Katoliki, Parokia mpya ya Mt. Bonaventure, Kinyerezi wakifuatilia ibada ya Krisamsi iliyokuwa ikiendeshwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kadinali Pengo (hayupo pichani), Dar es Salaam leo.
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Muadhama Polycarp Kadinali Pengo, akipokea michango mbalimbali ya fedha kutoka kwa viongozi wa Jumuiya za Kikristo katika jimbo la Segerea, Dar es Salaam, alipokwenda kuongoza ibada ya Krismasi sambamba na uzinduzi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mt. Bonaventure, Kinyerezi, Dar es Salaam leo. (Picha zote kwa hisani ya Habari Mseto Blog)

No comments:

Post a Comment