Liverpool ambayo mwenendo wake katika ligi kuu ya England umekuwa wa kusuasua, katika mechi yao ya Jumapili kwenye uwanja wa QPR, waliwacharaza wenyeji mabao 3-0.
Mshambuliaji machachari wa Liverpool ndiye ayelikuwa mwiba kwa vijana wa Harry Redknapp pale alipoifungia timu yake la Liverpool magoli mawili katika kipindi cha kwanza cha mchezo ikiwa ni katika dakika ya 10 na 16, huku Agger akiihakikishia Liverpool ushindi wa pointi tatu pale alipofyatua bao la tatu katika dakika ya 28 ya mchezo.
Kwa matokeo hayo Liverpool imejisogeza hadi nafasi ya 9 ikiwa na pointi 28 katika mechi 20 ilizocheza, na kuonyesha dhamira ya kurejea katika ubora wao wa zamani kwa kuwa miongoni mwa timu nne za England zinazowania kushiriki michuano mikubwa ya bara la Ulaya.
Kwa idadi hiyo hiyo ya mechi QPR wana pointi 10 tu, hali inayotishia kuendelea kuwepo kwao katika ligi kuu ya England msimu ujao
No comments:
Post a Comment