Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua mradi wa madawati kwa kukata utepe katika Kijiji cha Inyoga, Katavi. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Dk. Rajabu Rutengwe na kushoto ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Inyogo, Athony Kanyika. Waziri Mkuu Pinda, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Katavi yupo katika ziara ya jimbo hilo kwa kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amepewa heshima ya kimila kwa kuvishwa kofia na kukabidhiwa mkuki na wazee wa Inyonga kama ishara ya kutambua mchango wake kwa wananchi wa Mkoa huo wa Katavi kwa juhudi zake za kuwaletea maendeleo. Waziri Mkuu Pinda, ambaye ni Mbunge wa Jimbo hilo, yupo katika ziara jimboni mwake humo kukagua miradi mbalimbali na kuhamasisha maendeleo. (Picha zote na Chris Mfinanga)
No comments:
Post a Comment