Bendi ya muziki ya dansi ya Sky Light
ikitumbuiza katika sherehe za kutimiza miaka 20 ya Club Bilicanas na miaka 13 ya
Clouds FM.
Sherehe hizo zilipambwa na shamrashamra za aina
mbalimabli ikiwemo kukata keki pamoja na kufungua shampeni.
Mkurugenzi wa Club Billicanas Dk. Lilian Mtei akizungumza katika hafla
hiyo.
Mwakilishi wa Clouds FM, Wasiwasi Mwabulambo
akizungumza katika hafla hiyo.
Tukate keki
Mmoja kati ya
wafanyakazi wa kwanza wakati Bilicanas Club inaanzishwa miaka 20 iliyopita,
Monica Victor akimlisha keki, Mkurugenzi Dk. Lilian Mtei wakati wa hafla ya kutimiza miaka
20 ya klabu hiyo, iliyofanyika jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia
leo.
Maandalizi ya keki.
Pili Mitemo ambaye alimwakilisha mumewe,
aliyekuwa Meneja wa kwanza wa klabu hiyo, ambaye kwa sasa ni marehemu akipokea
keki kutoka kwa Mkurugenzi Dk. Lilian Mbowe kwa ajili ya kuwapa wadau waliojitokeza katika
hafla hiyo.
Mzee Ali Ramadhan Mkude naye akuwa mbali katika
mnuso wa Bilicanas Club kutimiza miaka 20 tangu kuanzishwa
DJ Ibrahim Tuwa 'Dj Ibra' akilishwa keki wakati
wa hafla hiyo
Dk. Lilian Mtei akimlisha kipande cha keki
Meneja Msaidizi wa Vinywaji wa Club Bilicanas, Amandus Agant wakati wa Birthday
ya Bilicanas Club kutimiza miaka 20.
Monica Victor akigawa keki kwa wadau waliofika
katika sherehe hizo.
Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka akiwa na
mmiliki wa blog ya Bongoweekend, Khadija Kalili pamoja na wadau wengine.
Watu wa mataifa mbalimbali
wakicheza muziki katika ukumbi wa Bilicanas. (Picha zote na Habari Mseto Blog)
Na Andrew
Chale
WADAU mbalimbali wa
burudani usiku wa kuamkia jana walifurahia kwa pamoja na kula keki ya miaka
20 ya klabu ya Kimataifa ya Bilicanas na miaka 13, ya Clouds Fm, iliyoambatana
na shamrashamra mbalimbali ndani na nje ya ukumbi huo.
Sherehe hizo ziliongozwa na
Mkurugenzi Mtendaji wa Bilicanas Group, Dk. Lilian Mtei ambapo aliwashukuru
wadau hao kwa kuwa bega kwa bega na klabu hiyo, tangu 1992. “Tunawashukuru sana
kwa kuwa nanyi mara zote inatia faraja kwetu na tutaendelea kutoa huduma bora
siku zote|” alisema Mbowe.
Mtei pia aliwashukuru
wafanyakazi mbalimbali waliofanikisha ukumbi huo kufikia hapo na kutoa heshima
ya kipekee kwa wafanyakazi waliokuwapo tokea inaanza hadi ilipofikia miaka 20
na hatimaye kukata keki hiyo.
“Uwepo wa miaka 20, tuna kila
sababu ya kuwapongeza wafanyakazi tuliokuwa nao toka mwanzo hadi leo, na kwa
heshima ya pekee Mama Victor na Mrs Mitemo ndiyo watakao kata keki hii”
alisema Mtei.
Keki hiyo ilikatwa na
wafanyakazi hao Monica Victor na Pili Mitemo ambaye alimwakilisha mumewe
aliyekuwa Meneja wa kwanza wa klabu hiyo, ambaye kwa sasa ni
marehemu.
Aidha, kwa upande Clouds FM,
iliwakilishwa na Wasiwasi Mwabulambo ambaye alipongeza klabu Bilicanas kwa kuwa
mstari wa mbele katika kuinua sanaa nchini hasa kwa kuwasaidia wasaidia wasanii
kufikia malengo yao.
Kwa upande wake Ibrahim Tuwa
‘Dj Ibra’ aliyekuwa akisherehesha shughuli hiyo, aliwaomba wadau kuendelea
kuwaunga mkono na wataendelea na huduma bora zaidi ha hapo. Dj Ibra alijiunga na
Bilicanas tokea 2002,ambapo mpaka sasa ana miaka 10 kwenye klabu hiyo iliyowahi
kuwa na madj maarufu waliopita hapo ambao wengi wao wapo kwenye vituo vya
televisheni na redio.
No comments:
Post a Comment