Bi. Zippora Shekilango ambaye ni mwasisi wa mtaa wa Shekilango jijini Dar es Salaam, akichangia mada leo katika ukumbi wa Ubungo Plaza juu ya Kiswahili kutumika kama lugha ya Taifa katika katiba ijayo, wakati wa warsha ya maandalizi ya Tamasha la Azaki za Kiraia Tanzani litakalo anza kesho jijini. (Picha na Francis Godwin)
Na Francis Godwin
WASHIRIKI wa Azaki za kiraia Tanzania wamependekeza katiba ijayo kuhakikisha lugha ya Kiswahili inakuwa ni lugha ya Taifa badala ya kuendelea kuliingiza Taifa katika utumwa wa kutumia lugha ya kiingereza .
Kwani wamedai kuwa lugha ya kigeni ndio imekuwa ikizidi kuwapa mwanya wageni na watu wachache wanaofahamu vema lugha ya kiingereza kujinufaisha na raslimali za Taifa kwa mikataba isiyoeleweka kwa wananchi wasioelewa lugha hiyo ya kiingereza.
Akichangia mada juu ya mtazamo wa azaki za kiraia kuhusu elimu ya Tanzania leo, wakati wa mafunzo ya siku mbili ya maandalizi ya tamasha la mwaka la azaki za kiraia warsha inayoendelea katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam Zippora Shekilango ambaye ni mwasisi wa mtaa wa Shekilango jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa wakati baadhi ya nchi dunia kama China na Uingereza wananufaika na lugha za mataifa yao katika kukuza ajira na kuongeza kipato cha Taifa kwa kuwa na wakalimani wengi wa lugha ya kwao ,Tanzania tumeendelea kujitumikisha kwa kuikumbutia lugha ya kigeni na kuipa mgongo lugha ya kishwahili ambayo ni lugha yetu .
Hivyo alisema lazima sasa Tanzania kusimama imara katika kutetea lugha yetu ikiwa ni pamoja na kuwa ni lugha ya kufundishia mashuleni badala ya kutumia lugha ya kiingereza kama ni lugha ya kufundishia mashuleni.
Hivyo alitaka katika katiba ijayo kuhakikisha suala la lugha ya Kiswahili kupewa kipaumbelea zaidi japo wananchi hawatazuiwa kujifunza lugha nyingine huku Kiswahili kikibaki kama ni lugha ya Taifa na si vinginevyo.
Mshiriki kutoka kundi la vyombo vya habari Tanzania Henry Muhanika alisema kuwa ili kuhakikisha lugha ya Kiswahili linapewa kipaumbele katika Taifa ni vema kuingizwa rasmi katika katiba ijayo ili kuenzi utamaduni wetu.
Hivyo alisema lazima kuwekeza zaidi katika utamaduni wetu kama watanzania kwa kutumia lugha yetu ya Kiswahili badala ya kuendelea kukubali kuwa watumwa katika Taifa kwa kuipa nafasi lugha ya kigeni katika Taifa huru.
Kwa upande wake mkurugenzi wa chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania (TAMWA),Valeria Msoka alisema kuwa ni vema katiba ijayo kutamka wazi juu ya Kiswahili kuwa ni lugha ya Taifa .
Alisema kuwa serikali ni lazima kuweka msukomo wa kipekee katika kuwekeza zaidi katika lugha ya Kiswahili ili kujinasua na utumwa wa kutumia lugha za kigeni zaidi.
Kwani alisema inashangaza kuona Tanzania ikiendelea kukumbatia lugha ya kigeni wakati baadhi ya nchi zikikwepa kutumia lugha hiyo ya kiingereza.
Katika hatua nyingine Msoka alipendekeza kuwa katiba ijayo mbali ya lugha ya Kiswahili kupewa kipaumbele bado suala la kijinsia katika katiba ijayo ni lazima kupewa kipaumbele zaidi.
No comments:
Post a Comment