WAREMBO
wanaoshiriki mashindano ya Miss East Africa 2012 wanatarajiwa kuanza kuwasili
kesho jijini Dar es salaam wakitokea katika Nchi mbalimbali tayari kwa
mashindano hayo makubwa yatakayo fanyika tarehe 07 December katika ukumbi wa
Mlimani City jijini Dar es salaam
wakati
huo huo Mtangazaji mashuhuri wa Mnet na ambae amewahi kuwa mshindi wa Big
Brother Africa, Gaetano Kagwa anayeishi Afrika Kusini ndiye atakaekuwa MC wa
mashindano ya mwaka huu ya Miss East Africa 2012 yatakayofanyika jijini dar es
salaam
Fainali
za mashindano ya Miss East Africa 2012 zitashirikisha warembo kutoka Nchi za
Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Djibouti, Eritrea, Sudan,
Ethiopia, Malawi, Madagascar, Reunion, Comoros, Seychelles, na Mauritius na
warembo mbalimbali wa Afrika mashariki walioshindana katika Nchi mbalimbali za
Ulaya
Mashindano
ya Mwaka huu yanayosubiliwa kwa hamu yanatarajiwa kushuhudiwa na mamilioni ya
watu Duniani kupitia kwenye luninga zao na pia kwa njia ya Internet ambapo
yatautangaza utalii wa Tanzania kwa kiasi kikubwa na pia kujenga umoja wa Afrika
mashariki na kudumisha utamaduni wa ukanda huu wa Afrika.
Mashindano
ya Miss East Africa yanaandaliwa na kumilikiwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya
jijini Dar es salaam

No comments:
Post a Comment