Watuhumiwa wa kesi ya mauaji ya Swetu Fundikira, Koplo Ally Ngumbe (kushoto), Koplo Mohammed Ally (katikati) na Sajenti Rhoda wakisikiliza hukumu ya kesi yao, waliyohukumiwa kunyongwa hadi kufa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Koplo Ally Ngumbe (kushoto), Koplo Mohammed Ally (kulia), wakisindikizwa na Askari Magereza kuelekea gerezani kusubiri hukumu ya kunyongwa hadi kufa iliyotolewa dhidi yao na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam jana baada ya kukutwa na hatia ya mauaji ya Swetu Fundikira.
Baadhi ya ndugu wa wanajeshi waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa, wakilia kwa uchungu baada ya kutolewa hukumu hiyo kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam jana.
Mmoja wa ndugu hao, akipewa huduma ya kwanza baada ya kuzirai kutokana na mshtuko wa hukumu hiyo. (Picha Francis Dande wa Habari Mseto)

No comments:
Post a Comment