TANGAZO


Sunday, November 11, 2012

Vodacom yamwaga mikopo ya milioni 17 Buigiri, Dodoma


Mwanachama wa kikundi cha Upendo katika kijiji cha Buigiri mkoani Dodoma, Diria Yaledi Mtumwa (kushoto), akipokea fedha ikiwa ni mkopo uliotolewa na Kampuni ya simu ya mkononi ya Vodacom kwa kupitia mpango wake wa Uwezeshaji kwa Wanawake kwa njia ya M-Pesa (MWEI). Mikopo ya jumla ya kiasi cha zaidi ya Sh. Milioni 17 ilitolewa kwa wanawake wa Buigiri na kukabidhiwa na Meneja wa Vodacom Foundation, Grace Lyon (kulia),huku Afisa wa Vodacom Ally Mbuyu (wa pili akishuhudia). Makabidhiano hayo ya awamu ya pili ya mikopo ya MWEI yalifanyika kijijini Buigiri mkoani Dodoma leo.
 
Mwanachama wa kikundi cha Upendo katika kijiji cha Buigiri mkoani Dodoma, Diria Yaledi Mtumwa (kushoto), akipokea fedha ikiwa ni mkopo uliotolewa na Kampuni ya simu ya mkononi ya Vodacom kwa kupitia mpango wake wa Uwezeshaji kwa Wanawake kwa njia ya M-Pesa (MWEI)
Mwanachama wa kikundi cha Upendo katika kijiji cha Buigiri mkoani Dodoma, Diria Yaledi Mtumwa (kushoto) akionesha fedha za mkopo alizokabidhiwa na kampuni ya simu ya mkononi ya Vodacom kwa kupitia Mpango wa Uwezeshaji kwa Wanawake kwa njia ya M-Pesa (MWEI). Zaidi ya Sh. Milioni 17 zilitolewa kwa wanawake wa kijiji cha Buigiri, mkoani Dodoma leo.
 
 
Maofisa wa Vodacom, wakiwa na wanawake wa Buigiri, mkoani Dodoma wakati wa hafla hiyo leo.

No comments:

Post a Comment