TANGAZO


Saturday, November 17, 2012

Ujumbe wa Tanzania na Malawi waamua kukubaliana kutokubaliana mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa, jijini Dar es Salaam

Baadhi ya wajumbe wa Malawi, wakijadiliana jambo, wakati ujumbe huo, ulipokutana jijini Dar es Salaam leo na ujumbe wa Tanzania kuzungumzia mpaka wa nchi hizo wenye utata kwenye Ziwa Nyasa.


Baadhi ya wajumbe wa Tanzania, wakijadiliana jambo, wakati ujumbe huo, ulipokutana jijini Dar es Salaam leo na ujumbe wa Malawi kuzungumzia mpaka wa nchi hizo mbili wenye utata kwenye Ziwa Nyasa. Wapili kushoto ni Mwanasheria wa Tanzania, Frederick Werema.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi, Mganda Chiume, akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, mara baada ya ujumbe wa nchi hiyo na Tanzania kumaliza mazungumzo kuhusu mpaka wa nchi hizo katika Ziwa Nyasa ambapo nchi zote mbili zilitoa  uamuzi wa kukubaliana kutokubaliana katika mjadala wao wa mpaka wa Ziwa Nyasa baina ya nchi hizo.


Wapigapicha wa vyombo mbalimbali vya habari nchini, wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi, Mganda Chiume (hayupo pichani), wakati alipokuwa akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, mara baada ya ujumbe wa nchi hiyo na Tanzania kumaliza mazungumzo kuhusu mpaka wa nchi hizo katika Ziwa Nyasa ambapo nchi zote mbili zilitoa  uamuzi wa kukubaliana kutokubaliana katika mjadala wao wa mpaka wa ziwa hilo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Bernard Membe, akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, mara baada ya ujumbe wa Malawi na Tanzania kumaliza mazungumzo ya kujadili kuhusu mpaka wa nchi hizo katika Ziwa Nyasa ambapo nchi zote mbili zilitoa uamuzi wa kukubaliana kutokubaliana katika mjadala wao wa mpaka baina yao.


Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Bernard Membe, akiwaeleza waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu makubaliano yao na ujumbe wa Malawi uliokuwa ukiongozwa  na Waziri wao wa Mambo ya Nje, Mganda Chiume, kuhusiana na mpaka wa Ziwa Nyasa ambapo nchi zote mbili zilitoa uamuzi wa kukubaliana kutokubaliana katika mjadala wao wa mpaka baina yao.


Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini, wakiandika maelezo kuhusu ufafanuzi uliokuwa ukitolewa na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Bernard Membe na wa Malawi, Mganda Chiume, Dar es Salaam leo, mara baada ya ujumbe wa nchi hizo, kumaliza mazungumzo ya kujadili kuhusu mpaka wa nchi hizo katika Ziwa Nyasa ambapo nchi zote mbili zilitoa uamuzi wa kukubaliana kutokubaliana katika mjadala wao huo.


Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Bernard Membe (kushoto) na Malawi Mganda Chiume (kulia), wakitoa maelezo kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, mara baada ya ujumbe wa nchi hizo mbili kutoa uamuzi wa kukubaliana kutokubaliana katika mjadala wao wa mpaka wa Ziwa Nyasa baina ya nchi hizo.

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Bernard Membe (kushoto) na Malawi Mganda Chiume (wa pili), wakitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam, mara baada ya ujumbe wa nchi hizo mbili kutoa uamuzi wa kukubaliana kutokubaliana katika mjadala wao wa mpaka wa Ziwa Nyasa baina ya nchi hizo.


Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi, Mganda Chiume, akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, mara baada ya ujumbe wa nchi hiyo na Tanzania kutoa uamuzi wa kukubaliana kutokubaliana katika mjadala wao wa mpaka wa Ziwa Nyasa baina yao.


Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Bernard Membe, akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, mara baada ya ujumbe wa Malawi na Tanzania kumaliza mazungumzo ya kujadili kuhusu mpaka wa nchi hizo katika Ziwa Nyasa ambapo nchi zote mbili zilitoa uamuzi wa kukubaliana kutokubaliana katika mjadala wao wa mpaka baina yao.


Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Bernard Membe, akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, mara baada ya ujumbe wa Malawi na Tanzania kumaliza mazungumzo ya kujadili kuhusu mgogoro wa mpaka wa nchi hizo katika Ziwa Nyasa ambapo nchi zote mbili zilitoa uamuzi wa kukubaliana kutokubaliana katika mjadala wao wa mpaka baina yao.

No comments:

Post a Comment