TANGAZO


Sunday, November 18, 2012

Serengeti Boys yaichapa moja bila, Congo Brazzaville, Dar es Salaam

Mchezaji Mohamed Hussein wa Serengeti Boys, akiudhibiti mpira huku akikabwa na Obassi Ngatsongo wa Congo Brazzaville, wakati timu hizo zilipopambana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo, kuwania kufuzu kwa fainali za 10 za Afrika kwa Vijana wa umri chini ya miaka 17 (U-17), zitakazofanyika nchini Morocco 2013. Serengeti ilishinda bao 1-0. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

Loussoukou Amour wa Congo Brazzaville, akituliza mpira huku akizongwa na Mohamed Salum wa
Serengeti Boys.

Ismail Adam wa Serengeti Boys, akiudhibiti mpira mbele ya Binguila Hordy wa Congo Brazzaville.

Mohamed Hussein wa Serengeti Boys akimtoka Obassi Ngatsongo wa Congo Brazzaville.

Mohamed Hussein wa Serengeti Boys akijaribu kutaka kumpiga chenga Obassi Ngatsongo wa Congo Brazzaville katika mchezo huo.

Obassi Ngatsongo wa Congo Brazzaville akikimbilia mpira baada ya Mohamed Hussein wa Serengeti kudondoka chini.

Obassi Ngatsongo wa Congo Brazzaville akiondoka na mpira huku akiangaliwa kwa makini na Selemani Hamis wa Serengeti Boys.

Mchezaji Obassi Ngatsongo wa Congo Brazzaville, akipambana na Selemani Hamis Bofu wa Serengeti Boys.

Mashabiki wa Tanzania wakifuatilia mchezo huo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni.


Kijana akiwa amevalia kinyago, akiishangilia na wenzake timu ya Serengeti Boys baada ya kuwa mbele kwa bao 1-0, kabla ya kumalizika kipindi cha kwa nza cha mchezo huo.

No comments:

Post a Comment