TANGAZO


Thursday, November 8, 2012

Rais Jakaya Kikwete azindua mradi wa ujenzi wa viwanda vya kusafisha gesi na bomba la kusafirishia, Kinyerezi jijini Dar es Salaam

Mwimbaji wa kundi la mipasho la Tanzania One Theatre (TOT), Khadija Kopa akiimba wimbo unaoitwa Mjini Chuo Kikuu, wakati kundi hilo lilipotumbuiza katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa viwanda vya kusafisha gesi asilia Mnazi Bay Mtwara, Songo Songo, Kilwa na uzinduzi wa bomba la kusafirishia gesi hiyo kuja Dar es Salaam katika kituo kikuu,
Kinyerezi jijini leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

 Kikosi cha bendi cha Jeshi la Kujenga Taifa kikitumbuiza, katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa viwanda vya kusafisha gesi asilia Mnazi Bay Mtwara, Songo Songo, Kilwa na uzinduzi wa bomba la kusafirishia gesi hiyo, kuja jijini Dar es Salaam katika kituo kikuu,
Kinyerezi jijini leo.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal (kulia), akizungumza jambo na Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Muhonga (katikati), wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa viwanda vya kusafisha gesi asilia Mnazi Bay Mtwara, Songo Songo, Kilwa na uzinduzi wa bomba la kusafirishia gesi hiyo, kuja Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mohammed Gharib Bilal (kulia mwenye miwani), akizungumza jambo na Balozi wa China nchini, Lu Youqing (wa pili kushoto), wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa viwanda vya kusafisha gesi asilia Mnazi Bay Mtwara, Songo Songo, Kilwa na uzinduzi wa bomba la kusafirishia gesi hiyo, kuja Dar es Salaam.
Rais wa Jakaya Kikwete (kushoto), akisalimiana na Makamu wake, Mohammed Gharib Bilal, wakati alipofika Kinyerezi kuzindua mradi wa ujenzi wa viwanda vya kusafisha gesi asilia Mnazi Bay Mtwara, Songo Songo, Kilwa na uzinduzi wa bomba la kusafirishia gesi hiyo, kuja Dar es Salaam.

Rais wa Jakaya Kikwete (kulia), akisalimiana na wananchi, wakati alipofika Kinyerezi kuzindua mradi wa ujenzi wa viwanda vya kusafisha gesi asilia Mnazi Bay Mtwara, Songo Songo, Kilwa na uzinduzi wa bomba la kusafirishia gesi hiyo, kuja Dar es Salaam.


Rais wa Jakaya Kikwete akiwapungia wananchi, wakati alipofika Kinyerezi kuzindua mradi wa ujenzi wa viwanda vya kusafisha gesi asilia Mnazi Bay Mtwara, Songo Songo, Kilwa na uzinduzi wa bomba la kusafirishia gesi hiyo, kuja Dar es Salaam.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto), akimweleza Rais Jakaya Kikwete katika michoro, kiasi cha uzalishaji na usafishaji wa gesi asilia kwa visima  vya Mnazi Bay, Mtwara na Songo Songo, Kilwa utakavyokuwa, wakati alipofika Kinyerezi jijini leo, kuzindua mradi wa ujenzi wa viwanda hivyo pamoja na bomba la kusafirishia gesi hiyo, kuja Dar es Salaam.
 Baadhi ya wananchi wakiwa katika hafla ya uzinduzi huo, Kinyerezi jijini Dar es Salaam leo.

 Baadhi ya Maofisa wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO), wakiwa katika hafla ya uzinduzi huo, Kinyerezi jijini Dar es Salaam leo. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Mahusiano wa shirika hilo, Badra Masoud.

Baadhi ya wataalamu wa Kichina, watakaoshughulika na mradi huo, wakiwa katika hafla ya uzinduzi, Kinyerezi Dar es Salaam leo. Mradi huo unaomilikiwa na Serikali kupitia Shirika lake la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC), kwa kiasi kikubwa umefadhiliwa na Serikali ya China.

Balozi wa China nchini, Lu Youqing, akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa viwanda vya kusafisha gesi asilia Mnazi Bay Mtwara, Songo Songo, Kilwa na uzinduzi wa bomba la kusafirishia gesi hiyo, kutoka Mtwara kuja Dar es Salaam.

Baadhi ya Wabunge wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa viwanda vya kusafisha gesi asilia Mnazi Bay Mtwara, Songo Songo, Kilwa na uzinduzi wa bomba la kusafirishia gesi hiyo, kutoka Mtwara kuja Dar es Salaam.

Baadhi ya waandishi wa habari, wakiwa kazini kuchukua matukio mbalimbali wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa viwanda vya kusafisha gesi asilia Mnazi Bay Mtwara, Songo Songo, Kilwa na uzinduzi wa bomba la kusafirishia gesi hiyo, kutoka Mtwara kuja Dar es Salaam.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Makamu wake, Dk. Mohamed Ghalib Bilali wakibadilishana mawazo, wakati  wa uzinduzi wa wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa viwanda vya kusafisha gesi asilia Mnazi Bay Mtwara, Songo Songo, Kilwa na uzinduzi wa bomba la kusafirishia gesi hiyo, kutoka Mtwara kuja Dar es Salaam.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, ambapo alifafanua mambo mbalimbali wanayokabiliana nayo katika utekelezaji wa mradi huo pamoja na faida zake kwa uchumi wa nchi na wananchi kwa ujumla.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akizungumza katika hafla ya kuuzindua mradi huo, Kinyerezi jijini Dar es Salaam leo, ambapo alieleza matumaini yake juu ya mradi huo kwa Taifa kwa takribani miaka 90 ijayo kutokana na uzalishaji wa gesi hiyo, aliyosema kuwa utawaondolea umasikini wananchi pamoja na kukuza pato la Taifa. 



Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akifunua pazi ili kuuzindua mradi huo, Kinyerezi jijini Dar es Salaam leo.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete (kulia), Makamu wake, Dk. Mohamed Ghalib Bilali (katikati) na Balozi wa China nchini, Lu Youqing (kushoto), wakipiga makofi baada ya Rais kuuzindua mradi huo, Kinyerezi jijini Dar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment