TANGAZO


Sunday, November 11, 2012

NMB, Kampuni ya Mantra Tanzania zadhamini maonesho ya Shule

 

 Maofisa wa Benki ya NMB, kutoka kushoto ni Monica Job, Simon Kameta na Germa Massawe, wakiwapa maelezo wananchi waliotembelea katika banda lao, kwenye Maonyesho ya Shule Tanzania, jijini Dar es Salaam leo.

Ofisa wa Benki ya NMB,  Monica Job, akimpatia maelezo mwananchi aliyetembelea katika banda hilo kwenye maonesho ya Shule Tanzania.

 Maofisa hao wa Benki ya NMB,  wakiwapa maelezo wanafunzi pamoja na wanchi waliotembelea banda la benki hiyo, kwenye maonyesho ya Shule Tanzania.

 Wakazi wa Dar es salaam, wakipata maelekezo kutoka kwa Maofisa wa Kampuni ya Mantra Tanzania Ltd. Kutoka kushoto ni Thobias Otaru na Nicholaus Masabo (wa pili), wakiwafahamisha jambo wananchi waliotembelea kwenye aonesho ya Shule yanayofanyika jijini Dar es Salaam. 

  Wakazi wa Dar es salaam, wakipata maelekezo kutoka kwa Maofisa wa Kampuni ya Mantra Tanzania Ltd, wakati wa Maonesho ya Shule yanayofanyika jijini Dar es Salaam. 

Banda la Mantra Tanzania Ltd, kwenye Maonesho ya Shule Jijini Dar es Salaam. (Picha zote na mpiga picha wetu)

No comments:

Post a Comment