Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo juu ya
ukarabati wa ukumbi wa mikutano wa 'White House' ulio katika Makao Makuu ya CCM,
mjini Dodoma ambao unafanyiwa ukarabati mkubwa ili kukidhi mahitaji ya sasa.
Rais Kikwete alisimama kwa muda mjini Dodoma jana, Jumanne Novemba 6, 2012,
akitoka katika ziara ya kikazi ya Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Singida,
alikokagua jumla ya miradi 19 ndani ya wiki moja.
Mwenyekiti wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akikagua maandalizi ya
ukumbi, utakaotumika wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM, ulio kwenye kitongoji cha Kizota mjini
Dodoma. Rais Kikwete alisimama kwa muda mjini Dodoma jana, Jumanne Novemba 6,
2012 akitoka katika ziara ya kikazi Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na
Singida alikokagua jumla ya miradi 19 ndani ya wiki moja.
Mafundi
rangi wakiwa kazini kuweka mambo sawa nje ukumbi, utakaotumika wakati wa Mkutano
Mkuu wa CCM ulio kwenye kitongoji cha Kizota mjini Dodoma
Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongiozi wengine wakipata maelezo
toka kwa Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama juu ya maandalizi ya ujenzi wa
Makao Makuu na vitega uchumi vya chama hicho, mjini Dodoma ambako. alisimama kwa
muda jana, Jumanne Novemba 6, 2012 akitoka katika ziara ya kikazi Mikoa ya
Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Singida alikokagua jumla ya miradi 19 ndani ya
wiki moja. (Picha zote na Ikulu)
No comments:
Post a Comment