TANGAZO


Monday, November 12, 2012

Mkutano wa kustawisha Huduma za Jamii na Utawala bora (AAPAM) kwa wafanyakazi Zanzibar

Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa Kustawi Huduma za Jamii na Utawala bora (AAPAM), wakiwa ukumbini, wakimsubiri mgeni rasmi, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, ambaye alimwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Sheni kabla ya kuwasili ukumbini huko Zanzibar Beach Resort.

Bendi ya Jeshi la Polisi, ikitumbuiza kwenye mkutano wa kustawi huduma za jamii na utawala bora (AAPAM), ukumbini wa Zanzibar Beach Resort, mjini humo leo.

Rais wa AAPAM,  Abdon Agaw Jok Nhial, akisalimiana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, mara baada ya kuwasili huko Zanzibar Beach Resort, nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Kulia kwa Makamu wa Rais  ni Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi, Zanzibar ambaye pia ni Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Rais wa AAPAM, Abdon Agaw Jok Nhial, akihutubia wajumbe wa Mkutano 34  juu ya suala zima la ustawi wa huduma za jamii na utawala bora huko Zanzibar Beach Resort. (Picha zote na Makame Mshenga Makame - Maelezo, Zanzibar)

No comments:

Post a Comment