TANGAZO


Monday, November 12, 2012

Mkutano Mkuu wa Nane wa CCM, Kizota Dodoma

Mwwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Rais Jakaya Kikwete akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Wilson Mukama, wakati wa mkutano huo leo. Katikati ni Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara anaye maliza muda wake, Pius Msekwa.


 Makada wa CCM wakiwa wabebeba masanduku ya kupigia kura.


 Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa nane wa Taifa wa Chama Cha Mapnduzi (CCM), wakiingia ukumbi wa Kizota mjini Dodoma leo, ikiwa ni siku ya pili tangua uanze mkutano huo jana.


Waziri asiye na Wizara maalumu, Profesa Mark Mwandosya, akitoka katika ukumbi huo, akiwa ameongozana na mkewe mama Mwandosya.


Mbunge wa Maswa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Shibuda akisalimiana na mke wa Rais mstaafu wa Zanzibar, Shadia Karume baada ya kumaliza kutoa pongezi kwa CCM kwenye mkutano huo leo.


Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akitoa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM kwa Serikali ya Muungano kwa mwaka 2007 na  2012.


 Wajumbe wa mkutano huo, wakifuatila matukio mbalimbali yaliyokuwa yakitendeka ukumbini humo.



Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, akisoma taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM ya Wizara yake kwa mwaka 2007/2012 kwenye mkutano huo leo. (PICHA ZOTE NA DOTTO)


Na Dotto Mwaibale, Dodoma
KITENDAWILI cha nani atachaguliwa kuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya  Chama Cha Mapinduzi (NEC-CCM),  kimetenguliwa baada ya vigogo kadhaa wa chama hicho  Tanzania Bara  ambao walikuwa kwenye upinzani mkali wa kuwania  ujumbe huo wa NEC kuibuka kidedea.
Miongoni mwa Mawaziri waliochomoza ni pamoja na Bernard Membe, Stephen Wassira, Dk. David Mathayo na Dk. Fenella Mukangara.
Katika uchaguguzi huo, uliokuwa na ushindani mkubwa, zaidi ya wagombea 31 waliteuliwa kuwania nafasi za ujumbe wa NEC, ambapo waliotakiwa walikuwa ni 10 pekee.
Habari kutoka ndani  chama hicho, za uhakika ingawa bado washindi hao hawajatajwa rasmi zimesema washindi hao walipata kura nyingi  kwa kupigiwa na  wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama hicho.
 Vigogo waliofanikiwa kuingia katika Halmashauri hiyo, wametajwa kuwa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu),  Stephen Wasira ambaye  amepata kura 2135, Naibu Waziri wa  Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia  January Makamba, aliyepata kura 2093.
Mawaziri wengine wametajwa kuwa ni Waziri wa Maendeleo ya Mifugo, Dk. David Mathayo aliyepata kura 1414 na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mkangara aliyepata kura  984.
Wengine ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi aliyepata kura 1805, Mbunge wa Iramba Magharibi na Katibu wa Uchumi na Fedha wa CCM, Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama aliyepata kura 1174.
Wengine, wametajwa  kuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Musoma,  Jackson Msome aliyepata kura 1207 na Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Martine Shigela 1824.
Wagombea ambao wanadaiwa kubwagwa ni Mbunge wa Afrika Mashairiki, Shy-Rose Bhanji, Hadija Faraji, Nicholaus Haule, Dk. Hussain Hassan, Rashid Kakozi, Twalhata Kakurwa na Godwin Kunambi.
Wengine ni Anna Magowa, mtoto wa mwasiasa mkongwe nchini, Wiliam Malecela, Salehe Mhando, Ruth Msafiri, Mbunge wa Nkenge, Assumpter Mshama, Kesi Mtambo na Christopher Mullemwah.
Wagombea wengine walioshindwa ni Mwanamanga Mwaduga, Fadhil Nkurlu, Innocent Nsena, Nussura Nzowa, Richard Tambwe na Tumsifu Mwasamale. 
Hata hivyo Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho, Rais Jakaya Kikwete alisema wajumbe wote 20, watakao shinda nafasi hizo 10 kutoka Zanziba na 10 wa Tanzania Bara na Mwenyekiti wa chama hicho na Makamu wake wawili kutoka Tanzania Bara na Zanzibar yatatajwa kesho baada ya kukamilika kwa uchaguzi huo.

No comments:

Post a Comment