TANGAZO


Monday, November 12, 2012

Amchoma mtoto kwa maji ya moto, amfungia ndani na kumlazimisha kula kinyesi



Mtoto aliyejulikana kwa jina moja la Aneti, akiwaonesha kidonda baadhi ya wakazi waliojitokeza kumwokoa baada ya kufungiwa ndani na mama yake mdogo huku akiwa amechomwa na maji ya moto na kulazimishwa kula kinyesi tukio ambalo lilitokea leo, Majengo jijini Mbeya. (Picha zote na Venance Matinya)


Msamaria mwema ambaye jina lake halikujulikana mara moja akimkimbiza hospitali mtoto Aneti aliyechomwa moto na mama yake mdogo, Bahati Lukangala katika tukio lililotokea leo, Majengo Jijini Mbeya.


Wakazi wa Kata ya Majengo, jijini Mbeya, wakiwa wamemshikilia Bahati Lukangala, wakimpeleka kituo cha Polisi, akituhumiwa kumchoma kwa maji ya moto mtoto wa dada yake, Aneti kisha kumfungia ndani na kumlazimisha kula kinyesi katika tukio lililotokea  leo mjini Mbeya.


Na Venance Matinya, Mbeya.


Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mkazi mmoja  wa mtaa wa Majengo, Kata ya Majengo jijini Mbeya, Bahati Rukangara amemchoma moto mtoto mdogo wa mika 3, aliyefahamika kwa jina moja  la Aneth kisha kumfungia ndani na kumlazimisha ale kinyessi chake.

Tukio hilo la kisikitisha lilitokea leo, majira ya saa nne asubuhi baada ya majirani kusikia yowe la mtoto huyo, akiomba msaada kutokana na mateso na maumivu makali aliyokuwa akiyapata kutokana na adhaabu hiyo kutoka kwa mama yake mdogo.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Mwenyekiti wa mtaa huo,   Habiba Mwakitabu alisema tukio hilo liligunduliwa na majirani na mwanamke huyo mara baada ya kusikia sauti ya mtoto huyo akilia kutokana na maumivu.

Alisema mara baada ya kusikia sauti hiyo, walifika eneo hilo na kuanza kumhoji ili kufahamu kiini cha tatizo hilo ambapo  alishindwa kutoa ushirikiano, ndipo walipoamua  kumpiga  hali ambayo haikusaidia kitu.

Alisema kutokana na hali hiyo, majirani walilazimika kubomoa mlango kutokana na mwanamke huyo kugoma kufungua ndipo walipo mkuta mtoto huyo akiwa uchi huku ameungua vibaya mwilini hasa katika upande mmoja eneo la mkono wa kushoto .

Mwenekiti huyo alisema mara baada ya kumhoji mtoto huyo aliwaeleza kuwa mama yake mdogo alichukua nguo na kumfunga mkononi kisha kumwagia maji ya moto pamoja na kumlazimisha ale kinyesi chake hali ambayo iliyosababisha kupiga kelele kwa lengo la kuomba msaada kwa watu wengine.

Kwa mujibu maelezo ya mwenyekiti huyo alisema kuwa Mtuhumiwa huyo amekuwa akifanya vitendo vya manyanyaso kwa mtoto huyo mara kwa mara ambapo wamekuwa wakimuonya lakini amekuwa si mtu wa kusikia.

Aliongeza kuwa mtoto huyo si wa kwake kwani amekuwa akiishi naye kwa muda mrefu sasa ambapo aliachiwa na dada yake ambaye hakufahamika kuwa anaishi wapi kwa sasa.

Kwa upande wake  Diwani wa kata hiyo  Samuel Mamboma alifika eneo hilo la tukio na kutoa msaada wa usafiri kwa lengo la kumfikisha mama huyo polisi pamoja na mtoto huyo ambaye naye alikimbizwa Hospitali.

Aidha aliwaonya wanawake kutowatesa watoto hao kutokana na kuharibu kizazi kijacho na kuwafanya watoto kuathirika kisaikolojia na kusababisha ongezeko la watoto wa mitaani wanaokimbia makwao kutokana na mateso ya wazazi wao.



No comments:

Post a Comment