TANGAZO


Monday, November 26, 2012

Makamu wa Rais, Dk. Bilal azindua mradi wa uimarishaji ajira kupitia mafunzo ya ufundi stadi VETA

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Elimu na Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa (wa pili kulia), wakikata utepe kwa pamoja kuashiria kuzindua jengo jipya la Ofisi za Veta, Mkoa wa Mtwara na Lindi, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Uimarishaji wa ajira kupitia mafunzo ya Ufundi Stadi katika Chuo cha Ufundi cha VETA mkoani Mtwara. Hafla hiyo, imefanyika leo Nov 26, 2012, mkoani humo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Simba Kalia, wa pili ni Mkurugenzi Mtendaji wa VETA nchini, Eng. Zebadia Moshi na kulia ni Mkuu wa Chuo cha VETA, Dar es Salaam, Idrisa Msholo. (Picha zote na OMR)
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa VETA nchini, Eng. Zebadia Moshi, wakati alipokuwa kitembelea na kukagua jengo jipya la VETA, lililopo mkoani Mtwara, baada ya kulizindua rasmi leo, Nov 26, 2012. Wa pili kushoto ni Mke wa Makamu wa Rais, mama Zakhia Bilal.
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa Uimarishaji wa ajira kupitia mafunzo ya Ufundi Stadi, Chuo cha Ufundi VETA mkoani Mtwara leo, Nov 26, 2012.
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa Uimarishaji wa ajira kupitia mafunzo ya Ufundi Stadi, Chuo cha Ufundi VETA mkoani Mtwara leo, Nov 26, 2012.
 
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwalimu wa Chuo cha VETA, Lupakisa Mapamba, kuhusu matumizi ya mashine ya kuchana mbao, wakati alipokuwa akitembelea katika Karakana za Chuo hicho, katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa Uimarishaji ajira kupitia Mafunzo ya Ufundi Stadi ya Chuo cha VETA, uliofanyika leo, Nov 26, 2012, mkoani Mtwara. Wa nne kushoto ni mke wa Makamu, mama Zakhia Bilal.

No comments:

Post a Comment