TANGAZO


Thursday, November 15, 2012

Kesi ya Sheikh Ponda na wenzake wasomewa mashtaka yanayowakabili Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam

Makomando wa Jeshi la Magereza wakiwa katika ulinzi Mahakama ya Kisutu, wakati kesi ya Sheikh Issa Ponda na wenzake ilipokuwa ikisomwa Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam leo. 

Askari Kanzu wakiwapekuwa wananchi waliokuwa wakiingia Mahakama ya Kisutu, kuasikiliza kesi ya Sheikh Issa Ponda na wenzake, Dar es Salaam leo.

Sheikh Issa Ponda na wenzake, wakiwa kwenye Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam leo kusomewa mashtaka yao yanayowakabili, yakiwemo ya kupora kiwanja, mali na uchochezi.

Baadhi ya wananchi, ndugu na marafiki wa washitakiwa katika kesi inayomkabili Sheikh Issa Ponda na wenzake, wakiwa kwenye Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam leo, kufuatilia kesi hiyo, ambayo baada ya kusomewa mashtaka hayo, iliaghirishwa hadi Novemba 29, mwaka huu. Kulia ni baadhi ya washtakiwa wa kesi hiyo. 

Sheikh Issa Ponda (kulia) na wenzake, wakiwa kwenye Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam leo kusomewa mashtaka yao yanayowakabili, yakiwemo ya kupora kiwanja, mali na uchochezi.

Mshitakiwa namba 5 katika kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Jumiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda (katikati) na wenzake, Mkadamu Saleh, akiteta, jambo na mmoja wa mawakili wao, Juma Nassoro, mara baada ya kusomewa mashtaka yao, kwenye Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam leo.

Askari Magereza, akimvalisha pingu Sheikh Issa Ponda, wakati wakijiandaa kuondoka mahakamani hapo baada ya kusomewa mashtaka yao.

Sheikh Issa Ponda (katikati), akiwa chini ya ulizi, wakati akiondoka mahakamani hapo kurejeshwa mahabusu baada ya kusomewa mashtaka yanayomkabili na wenzake. 

Baadhi ya wananchi, ndugu na marafiki wa washitakiwa katika kesi inayomkabili Sheikh Issa Ponda na wenzake, wakiwa kwenye Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam leo, kufuatilia kesi hiyo.

Askari Polisi na Magereza wakiwa katika ulinzi mkali Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam, wakati kesi ya Sheikh Issa Ponda na wenzake ilipokuwa ikisomwa leo. 

Askari Polisi na Magereza wakiweka ulinzi Mahakama ya Kisutu, wakati kesi ya Sheikh Issa Ponda na wenzake ilipokuwa ikisomwa leo. 

Askari Polisi wakiwa ndani ya gari lao pamoja na wenzao wa Magereza wakiwa katika ulinzi Mahakama ya Kisutu, wakati kesi ya Sheikh Issa Ponda na wenzake ilipokuwa ikisomwa leo. 


Msafara wa magari uliokuwa umembeba Sheikh Ponda na mwenzake, Mkadamu Saleh, ukiondoka katika Mahakama ya Kisutu.


Askari Magereza wakiwa katika gari lao wakiondoka Mahakama ya Kisutu na msafara uliokuwa umembeba Sheikh Issa Ponda na mwenzake, Mkadamu Saleh kurejeshwa mahabusu.

Polisi wakiwa kwenye gari leo, wakiondoka Mahakama ya Kisutu baada ya magari yaliyokuwa yamembeba Sheikh Issa Ponda na mwenzake, Mkadamu Saleh, kuondoka mahakamani hapo.



Gari la Polisi lenye maji ya kuwasha, likiondoka Mahakama ya Kisutu baada ya magari yaliyokuwa yamembeba Sheikh Issa Ponda na mwenzake, Mkadamu Saleh, kuondoka mahakamani hapo.

No comments:

Post a Comment