TANGAZO


Saturday, September 8, 2012

Wakazi wa Tabora wapagawa na Tamasha la Serengeti fiesta 2012



Mmoja wa wasanii mahiri katika miondoko ya hip hop nchini, Mwana FA, akiwaimbisha wakazi wa mji wa Tabora, wimbo wake wa Yalaiti, usiku wa kuamkia leo katika viwanja vya Ally Hassan Mwinyi, mjini humo, ambapo wakazi wa mji huo walijitokeza kwa wingi.Tamasha hilo, kesho litakuwa linarindima mjini Singida katika kiota cha maraha, kiitwacho Singida Motel.
 
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Mabeste akikamua kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012, usiku wa kuamkia leo, Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi, mjini Tabora, ambapo katika tamasha hilo wakazi wa mji huo, walijitokeza kwa wingi na kushuhudia vipaji mbalimbali vya muziki.
 
Mmoja wa wasanii waliokuwa wakishiriki kwenye tamasha hilo, akifanya makamuzi ya nguvu kwenye tamasha hilo.

 Wakazi wa Tabora walioamua kujiachia kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012, wakishangilia vilivyo burudani iliyokuwa ikitolewa na wasanii mbalimbali usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi, mjini Tabora, aidha tamasha hilo siku ya jumapili litakuwa linarindima ndani ya Singida Motel, mkoani humo.
 
Msanii Nikki Mbishi akishusha mistari yake mbele ya wakazi wa mji wa Tabota.
 
 Umati wa watu, wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
 
 Pichani kulia ni Shaffih Dauda,  akiwa na wadau mbalimbali.
 
 Wakazi wa mji wa Tabora, wakiwa ndani ya uwanja wa Ally Hassan Mwinyi, wakati wa tamasha la Serengeti Fiesa 2012, lilipokuwa linaondoka.
 
 Dj Zero kutoka Clouds FM, akikamua mashine na kulia kwake ni Hamza Bella.

 Moja wa zao la Serengeti Fiesta 2012, Supa Nyota "Ney Lee", akitumbuiza jukwaani.
 
Msanii Recho, akionesha umahiri wake wa kunengua jukwaani akisindikizwa madensa wake.
Mmoja wa wasanii, waliokuwa wakitumbuiza kwenye tamasha hilo, akifanya vitu vyake. Katika hali ya kawaida, palikuwa hapatoshi ndani ya Tabora usiku wa kuamkia leo.
 Rich Mavoko, akiliongoza skwadi lake kusakata kiduku.
 
 Mbunge wa Tabora mjini, Ismail Rage, akisoma moja ya namba ya mtu aliyebahatika kuibuka na bajaji. Kulia kwake ni Mkuu wa utafiti wa Clouds TV, Ruge Mutahaba.
 
 Ilikuwa ni  full mzuka mwanzo hadi mwisho kwa mashabiki.
 
Sir Juma Natura, akikamua usiku wa kuamkia leo kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012;
 
Watu walikuwa kibao kwenye tamasha hilo.
 
Hamza Bella na marafiki zake wakiwa wamepozi ndani ya tamasha la Fiesta 2012. usiku wa kuamkia leo. (Picha zote na mdau wetu)

No comments:

Post a Comment