TANGAZO


Monday, September 10, 2012

Toroka auaga ukapera

Bwana harusi, Eric Toroka akimvisha pete Bi. Joyce Mlaponi katika Ibada ya kufunga ndoa iliyofanyika kwenye Kanisa la Kiluteri la Msasani jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Bibi harusi, Joyce Mlaponi, akimvisha pete mumewe, Bwana Eric Toroka katika Ibada ya kufunga ndoa iliyofanyika Kanisa la Kiluteri la Msasani jijini hivi karibuni.

Bwana harusi, Eric Toroka akila kiapo cha ndoa wakati alipokuwa akifunga ndoa na Bi. Joyce Mlaponi (kulia), mbele ya usharika katika Ibada ya ndoa iliyofanyika Kanisa la Kiluteri la Msasani jijini hivi karibuni.

Bwana harusi, Eric Toroka na Bi. Joyce Mlaponi, wakiombewa baada ya kufunga ndoa katika Kanisa la Kiluteri la Msasani jijini hivi karibuni.

Bwana harusi, Eric Toroka, akimshika mkono mkewe Bi. Joyce Mlaponi, mara bada ya kufunga ndoa katika Kanisa la Kiluteri la Msasani, jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Ndugu wa Bw. Harusi Eric Toroka na Bi. Joyce Mlaponi, wakifuatilia Ibada ya ndoa iliyofanyika katika Kanisa la Kiluteri la Msasani, jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Bwana harusi Eric Toroka na mkewe, Joyce,  wakipokea cheti cha ndoa kutoka kwa mchungaji wa usharika wa Msasani jijini Dar es Salaam mara baada ya kufunga ndoa kanisani hapo hivi karibuni.

Maharusi, ndugu, jamaa na marafiki, wakipiga picha ya pamoja mara baada ya kufunga ndoa yao kwenye Kanisa la Kilutheri la Msasani jijini Dar es Salaam.

Bwana harusi Eric Toroka na mkewe, Joyce pamoja na wapambe wao, wakipiga picha kwenye fukwe za bahari ya Hindi mara baada ya kutoka Kanisani kufunga ndo yao, Msasani jijini Dar es Salaam.

Maharusi wakiwa na wazazi wa Bwana harusi, Eric Toroka pamoja na Bestman, Atuokoe Twite na Matron, Msunza Twite kwenye ufukwe wa Bahari ya Hindi, jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Bwana Harusi Eric Toroka akionesha mapenzi yake kwa mkewe kwenye fukwe za bahari ya Hindi wakokwenda kupunga upepo mara baada ya ndoa yao iliyofanyika kwenye Kanisa la Kilutheri la Msasani jijini Dar es Salaam.

Ni kama vile mama anasema mimi ni wako tu pekee wa kufa na kuzikana, hauna zaidi yako......

Ni kama vile bwana harusi, Toroka anamwambia mkewe, Bi. Joyce, 'leo nimekubamba, imefika arobaini yako, na huondoki peke yako, leo mimi na wewe tuu'.  

Bibi harusi akiwa na wakwe zake, Mama Juliana Toroka na shangazi 'Aunt ' Angela Sitati Toroka (kulia), kwenye fukwe za bahari hiyo.

Hebu na sisi tujikumbushe mwe. Wazazi wa Bwana harusi Eric Toroka, wakikumbuka enzi zao za kufunga ndo na pozi la harusi kwenye fukwe za Bahari ya Hindi.

Ndugu za Bi. Harusi Joyce, nao wakipata picha ya ukumbusho kwenye fukwe za Bahari ya Hindi, maeneo ya Coco Beach, jijini Dar es Salaam.

Maharusi wakisikiliza kwa makini maneno ya busara kutoka kwa baba mdogo wa Bwana harusi, Eric,  Epaineto Toroka, aliyekuwa akiwausia siku hiyo..



Hawa ndio wanakamati waliofanikisha shughuli yote na Bwana na Bi. harusi, Eric na Joyce Toroka, nao wakipata picha ya kumbukumbu kwenye ukumbi wa sherehe hiyo, Bwalo la Polisi, Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Leo ni kunyweshana na kulishana vitamu tu, haya ni maneno yaliyokuwa yakitolewa na maharusi hao wakati wakinyweshana mvinyo kwenye sherehe yao, ukumbini hapo.

Bwana na Bibi Harusi, Eric na Joyce, wakikata keki yao ya ndoa kwenye sherehe ya ndoa yao ukumbini humo. 

Graphic Designer wa Jambo Brand Tanzania Magazine, Betty Mkeleja akiwa na dada yake, Jane, wakishuhudia kwa makini sherehe za harusi ya Bwana Eric Toroka, ambaye ni Mhariri wa jarida hilo, linalotolewa na Kampuni ya Jambo Concepts ya jijini Dar es Salaam.

Hebu tuangalieni tulivyopendeza, haya ni maneno yaliyokuwa yakitolewa na maharusi hao, wakati wakipiga picha yao ya kumbukumbu ya ndo kwenye sherehe hiyo.

Maharusi Toroka na mkewe, Joyce wakifungua muziki kwenye Dance floor ya Bwalo la Polisi la Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Cheza Rhumba cheza Rhumba, leo cheza Rhumba, Bwana Harusi na Bi. harusi, Eric na Joyce wakizirudi ngoma wakati wa ufunguzi wa dansi ukumbini humo hivi karibuni. (Picha kwa hisani Eric Toroka)

No comments:

Post a Comment