TANGAZO


Thursday, September 6, 2012

Simba yakubali 3 kavu kwa Sofa Paka ya Kenya, Uwanja wa Taifa

Wachezaji wa timu za Simba ya Tanzania na Sofa Paka ya Kenya wakiingia Uwanja wa Taifa, kwa ajili ya mpambano wao wa kirafiki, Dar es Salaam leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

Wachezaji wa timu za Simba ya Tanzania na Sofa Paka ya Kenya wakisalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo wao wa kirafiki Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.

 Kikosi cha Simba kikipiga picha ya pamoja kabla ya kupambana na Sofa Paka ya Kenya, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.

Mchezaji Edward Christopher wa Simba (kulia), akijaribu kumtoka Anthony Kimani wa Sofa Paka wakati wa mchezo wa kirafiki wa Kimataifa kati ya timu hizo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.

 
Edward Christopher wa Simba (kulia), akimtoka Anthony Kimani wa Sofa Paka ya Kenya, wakati wa mchezo wa kirafiki wa Kimataifa kati ya timu hizo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.

 Daniel Akkufor wa Simba akichuana na Joseph Nyaga (anaye kwenda chini) wa Sofa Paka katika mchezo huo.

Mchezaji Daniel Akkufor wa Simba akiwa ameanguka chini na kuzimia baada ya kugongana na mwenzake wa Sofa Paka wakati wa mchezo huo.

Mchezaji Daniel Akkufor wa Simba akipatiwa huduma ya kwanza baada ya kuanguka chini na kuzimia baada ya kugongana na mwenzake wa Sofa Paka wakati wa mchezo huo.

Mchezaji Daniel Akkufor wa Simba akitolewa nje baada ya kupatiwa huduma ya kwanza baada ya kuanguka chini na kuzimia kutokana na kugongana na mwenzake wa Sofa Paka wakati wa mchezo huo.


Akkufor, akisaidiwa kutoka nje kwa ajili ya kupatiwa huduma zaidi.

Edward Christopher wa Simba (kulia), akimtoka Anthony Kimani wa Sofa Paka ya Kenya, wakati wa mchezo wa kirafiki wa Kimataifa kati ya timu hizo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.

Mchezaji Edward Christopher wa Simba (kulia), akijaribu kumtoka Pascal Ochieng wa Sofa Paka wakati wa mchezo wa kirafiki wa Kimataifa kati ya timu hizo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.

Mashabiki wa Simba wakifuatilia mchezo kati ya timu yao na Sofa Paka, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo.

Shomari Kapombe wa Simba, akitoa pasi kwa mwenzake (hayupo pichani), huku akifuatwa na Joseph Nyakii wa Sofa Paka katika mchezo huo.

Abdalla Juma wa Simba, akijaribu kuudhibiti mpira huku akifuatwa na George Owino wa Sofa Paka, hadi wakati huo, Simba ilishafungwa mabao 3-0.


Mwisho wa mchezo huo, ubao wa matokeo ukionesha Simba 0 na Sofa Paka 3.

No comments:

Post a Comment