TANGAZO


Thursday, September 6, 2012

Mbunge Zungu afungua Bonanza la Matumaini Jangwani

 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Jangwani, akimkaribisha diwani wa Jangwani Kariakoo, jijini Dar es Salaam ili na yeye amkaribishe Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan 'Zungu' kwa ajili ya kuzungumza na wachezaji wa timu mbalimbali za maeneo ya Ilala, wakati alipokuwa akilifungua bonanza la Matumaini, Dar es Salaam jana.

 Wachezaji wa timu za Bom Bom ya Ilala na Nungu ya mtaa wa Jangani, wakimsikiliza Mbunge Zungu wakati alipokuwa akizungumza kwenye ufunguzi wa Bonanza la Matumaini, wakati alipokuwa akilifungua, Dar es Salaam jana. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

 Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu, Wilaya ya Ilala, Daud Kanuti akizungumza na wachezaji pamoja na wananchi mbalimbali waliofika kwenye uzinduzi wa Bonanza la Matumaini, Viwanja vya Jangwani Dar es Salaam jana.


 Diwani wa Kata ya Jangwani, ambaye pia ni Meya mstaafu wa Ilala, Abuu Juma, akizungumza na wachezaji wa timu za Nungu na Bom bom zote za Ilala, wakati akilifungua Bonanza la Matumaini, Dar es Salaam jana.

 Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan 'Zungu', akisalimiana na wachezaji wa timu za Bom Bom na Nungu wakati alipokuwa akizikagua kabla ya mchezo wa ufunguzi wa Bonanza la Matumaini, Viwanja vya Jangwani Dar es Salaam jana.

 Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan 'Zungu', akisalimiana na wachezaji wa timu za Bom Bom na Nungu wakati alipokuwa akizikagua kabla ya mchezo wa ufunguzi wa Bonanza la Matumaini, Viwanja vya Jangwani Dar es Salaam jana.

Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu, akizungumza na mshambuliaji wa timu ya Bom Bom, Hisam Msema, wakati wa uzinduzi huo, Dar es Salaam jana.

Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu, akifanya usafi wa kuokota vipande vya chupa pamoja na vijiwe kwenye uwanja wa Jangwani kabla ya mchezo wa kombe la Bonanza la Amani kati ya timu za Bom Bom kupambana kwenye bonanza la Matumaini, Viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam jana.

Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu, akizungumza na mshambuliaji wa kike wa timu ya Bom Bom, Hisam Msema, wakati wa uzinduzi huo, Dar es Salaam jana.

Baadhi ya waandishi wa habari wa gazeti la Mseto, wakipiga picha ya pamoja mara baada ya kuzinduliwa bonanza la Matumaini na Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu, Viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam jana.

Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu, akizindua Bonanza la Matumaini kwenye viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam jana, kabla ya mechi ya ufunguzi kati ya timu ya Bom Bom na Nungu za jijini.
 
Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Zungu, akikagua nyavu za magoli kabla ya mchezo wa ufunguzi wa bonanza la Matumaini kuanza kati ya timu za Boom Bom na Nungu haujaanza jana.

No comments:

Post a Comment