TANGAZO


Thursday, September 20, 2012

Rais Kikwete azindua ujenzi wa Daraja la Kigamboni


 
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara (kushoto), akiwa na baadhi ya wananchi, wakicheza ngoma ya kabila la Wasukuma wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa Daraja la Kigamboni, maeneo ya Kurasini Dar es Salaam leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara (wa nne kushoto), akiwa na baadhi ya waataalamu wa ujenzi wa daraja hilo kutoka China na wananchi, wakicheza ngoma ya kabila la Wasukuma wakati wa uzinduzi wa ujenzi, maeneo ya Kurasini Dar es Salaam leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

 Baadhi ya wananchi wakiwa wamekaa chini kutokana na kusongamana na nafasi kuwa ndogo kwenye eneo la uzinduzi, Kurasini jijini Dar es Salaam.

 Baadhi ya wananchi pamoja na watoto, wakiangalia picha mbalimbali za michoro ya daraja hilo pamoja na njia zake kwenye mabango yaliyowekwa katika eneo hilo, wakati wa uzinduzi wa ujenzi, uliofanywa na Rais Jakaya Kikwete.

 Hii ni picha ya mchoro wa Daraja la Kigamboni litakavyokuwa baada ya ujenzi wake.

 Wananchi mbalimbali wakicheza ngoma za rusha roho, zilizokuwa zikipigwa kabla ya kuwasili kwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Rais Jakaya Kikwete.

 Baadhi ya Wabunge na wananchi mbalimbali, wakicheza ngoma za mduara kabla ya uzinduzi huo, kushoto ni Mbunge wa Kinodononi jijini Dar es Salaam, Mussa Azzan.

 Baadhi ya waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari, wakiwa wamekaa makini kwa ajili ya kufuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakitokea kwenye uzinduzi huo.

 Mmoja wa wapuliza tarumbeta wa kundi la Usambara Moutain, Rukia Madjid, akionesha ufundi na mbwembwe zake wa kupuliza chombo hicho, wakati kundi lake lilipokuwa likitoa burudani kwa wananchi na wageni mbalimbali waalikwa katika hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa Daraja hilo.
 Sehemu ya Daraja la muda litakalotumika kwa ajili ya kupitishia vifaa vya ujezi wa Daraja la Kigamboni likiwa linaendelea kujengwa kwa ajili ya kuanza shughuli rasmi za ujenzi wa Daraja la Kigamboni.

 Eng. Patrick Mfugale, kutoka Tanroad (kulia), akimweleza Rais Jakaya Kikwte michoro ya jinsi ya daraja hilo pamoja na njia zake zitakavyokuwa baada ya kukamilika ujenzi wake.
 
 Rais Jakaya Kikwete akiwa na Waziri wa Ujenzi, John Magufuli (kulia), wakielekea katika sehemu yake aliyopangiwa, wakati alipokuwa akiwasili maeneo hayo, tayari kwa shughuli za uzinduzi wa ujenzi wa daraja hilo.

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadiq, akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa daraja hilo.

 Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhan Dau, ambao ni wamiliki wa hisa za asilimia 60 katika ujenzi wa daraja hilo, akizungumza katika hafla hiyo.

 Wasanii wa kundi la JKT, wakicheza ngoma ya Kibati ya asili ya watu wa Pemba, wakati wa hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa daraja hilo.

 Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa daraja hilo.

 Rais Jakaya Kikwete, akizungumza na wananachi pamoja na wageni mbalimbali wakati alipofika katika eneo hilo kwa ajili ya kuzindua na kuweka jiwe la msingi wa ujenzi wa daraja hilo.

 Baadhi ya madiwani wa jiji la Dar es Salaam pamoja na wananchi na baadhi ya wageni mbalimbali wakiwa katika uzinduzi huo.

Rais Jakaya Kikwete akiweka jiwe la msingi kuashiria kuzindua rasmi ujenzi wa Daraja la Kigamboni katika hafla iliyofanyika huko Kurasini jijini Dar es Salaam leo mchana. Kushoto ni Waziri wa Ujenzi Dk John Pombe Magufuli na wa pili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dk Ramadhani Dau. NSSF itagharamia asilimia 60 za ujenzi wa daraja hilo na serikali asilimia 40 (Picha na Freddy Maro)

Rais Jakaya Kikwete akipiga makofi baada ya kuweka jiwe la msingi ikiwa kama ni uzinduzi rasmi wa ujenzi wa Daraja la Kigamboni, maeneo ya Kurasini jijini Dar es Salaam leo mchana. Kushoto ni Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka na katikati ni Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli. Ujenzi wa daraja hilo, utagharamiwa na Mfuko wa NSSF kwa asilimia 60 na serikali asilimia 40 (Picha na Kassim Mbarouk)

No comments:

Post a Comment