TANGAZO


Monday, September 10, 2012

Rais Jakaya Kikwete azindua Chuo cha Ulinzi cha Taifa, Dar es Salaam

 Rais Jakaya Kikwete, akikata utepe ili kuzindua Chuo cha Ulinzi cha Taifa cha Jeshi la Wananchi (JWTZ), Kunduchi jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Balozi wa China nchini, Lu Yu Qing, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha, Mkuu wa Majeshi Brigedia Jenerali Davies Mwamunyange na Mkuu wa Chuo hicho, Meja Jenerali Charles Makakala. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

 Rais Jakaya Kikwete, akipiga makofi pamoja na Balozi wa China nchini, Lu Yu Qing (wa pili kushoto), Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha na Mkuu wa Majeshi, Brigedia Jenerali Davies Mwamunyange, wakati alipokuwa akikizindua Chuo cha Ulinzi cha Taifa cha Jeshi la Wananchi (JWTZ), Kunduchi jijini Dar es Salaam leo. 

Rais Jakaya Kikwete, akiteta jambo na Mkuu wa Majeshi, Brigedia Jenerali Davies Mwamunyange (kushoto) na Mkuu wa Chuo hicho, Meja Jenerali Charles Makakala (katikati), wakati alipokuwa akikizindua Chuo hicho.

Rais Jakaya Kikwete, akizungumza na maofisa wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), wageni mbalimbali waalikwa pamoja na Balozi  na Maofisa wa Ubalozi wa China waliopo nchini, wakati alipokuwa akikizindua Chuo hicho, Dar es Salaam leo.

Mkuu wa Majeshi, Brigedia Jenerali Davies Mwamunyange (kushoto) na Mkuu wa Chuo hicho, Meja Jenerali Charles Makakala, wakimsikiliza Rais Jakaya Kikwete (hayupo pichani), wakati alipokuwa akikizindua Chuo hicho, cha Ulinzi cha Taifa, Dar es Salaam leo.

 Baadhi ya Maofisa mbalimbali wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), wakimsikiliza Rais Jakaya Kikwete (hayupo pichani), wakati alipokuwa akikizindua Chuo cha Ulinzi cha Taifa, Dar es Salaam leo.

Rais Jakaya Kikwete, akizungumza na maofisa wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), wageni mbalimbali waalikwa pamoja na Balozi  na Maofisa wa Ubalozi wa China waliopo nchini, wakati alipokuwa akikizindua Chuo hicho pamoja na kozi ya kwanza ya chuo, Kunduchi, jijini Dar es Salaam leo.


 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha (kushoto) na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Emmanuel Nchimbi, wakimsikiliza Rais Jakaya Kikwete (hayupo pichani), wakati alipokuwa akikizindua Chuo cha Ulinzi cha Taifa, Dar es Salaam leo.

Rais Jakaya Kikwete, akizungumza na maofisa mbalimbali wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), wageni mbalimbali waalikwa pamoja na Balozi  na Maofisa wa Ubalozi wa China waliopo nchini, wakati alipokuwa akikizindua Chuo hicho.

 Baadhi ya Maofisa mbalimbali wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), Polisi, Magereza na wageni mbalimbali waalikwa, wakimsikiliza Rais Jakaya Kikwete (hayupo pichani), wakati alipokuwa akizungumza katika uzinduzi wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa, Dar es Salaam leo.

Rais Jakaya Kikwete, akimkabidhi funguo ya Chuo, Mkuu wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa (NDC) cha Jeshi la Wananchi (JWTZ), Meja Jenerali Charles Makakala (kulia), ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa chuo na kozi ya kwanza ya jeshi hilo chuoni hapo.

Mkuu wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa (NDC) cha Jeshi la Wananchi (JWTZ), Meja Jenerali Charles Makakala, akiuonesha ufunguo huo, aliokabidhiwa na Rais Jakaya Kikwete (kushoto), ambao ni kama ishara ya uzinduzi wa chuo na kozi ya kwanza ya jeshi hilo chuoni hapo.

 Baadhi ya wanafunzi wa kwanza wa Chuo hicho, wakitoa heshima zao kwa Rais Jakaya Kikwete (hayupo pichani), wakati wa uzinduzi huo leo.

 Mkuu wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa (NDC) cha Jeshi la Wananchi (JWTZ), Meja Jenerali Charles Makakala, akimueleza jambo Rais Jakaya Kikwete, mara baada ya kukizindua Chuo hicho cha Ulinzi cha Taifa na kozi ya kwanza ya chuo leo. Kushoto ni Mkuu wa Majeshi, Brigedia Jenerali Davies Mwamunyange. 

 Rais Jakaya Kikwete (katikati), akiwa na baadhi ya wanafunzi wa kwanza wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa, mara baada ya kukizindua, Dar es Salaam leo.

Rais Jakaya Kikwete, akiteta jambo na mmoja wa wageni waalikwa katika uzinduzi wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa (NDC) cha Jeshi la Wananchi (JWTZ), Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi kwenye uzinduzi wa chuo hicho.

Wasanii wa kundi la Jeshi la Wananchi (JWTZ), wakicheza ngoma za kabila la Kisukuma, mbele ya Rais Kakaya Kikwete, wakati wa uzinduzi wa Chuo hicho pamoja na kozi ya kwanza ya Chuo, Dar es Salaam leo.

1 comment: