TANGAZO


Tuesday, September 11, 2012

Lowassa akabidhi madawati 500 Shule ya Msingi Minazi Mirefu

 Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, akikata utepe wakati alipokabidhi madawati 500 kwa shule ya Msingi Minazi Mirefu, Ukonga jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mahusiano ya Serikari wa Kampuni ya African Barrick Gold, Emmanuel Ole-Naiko.

 Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa akimkabidhi cheti, Mkurugenzi wa Mahusiano ya Serikari wa Kampuni ya African Barrick Gold, Emmanuel Ole-Naiko, wakati wa hafla ya kukabidhi madawati 500 katika Shule ya Msingi Minazi Mirefu, Ukonga jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa akizungumza jambo na wanafunzi wa Shule ya Msingi Minazi Mirefu, mara baada ya kukabidhi madwati 500 kwa shule hiyo, Ukonga jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Mahusiano ya Serikari wa Kampuni ya African Barrick Gold, Emmanuel Ole-Naiko.


 Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa akizungumza katika hafla hiyo. (Picha na mdau wetu)

 Naibu Waziri wa Kazi na Ajira na Mbunge wa Jimbo la Segerea,Mh. Makongoro Mahanga akizungumza machache na kutambulisha baadhi ya wageni waliohudhulia katika hafla hiyo fupi ya kukabidhi madawati 500 kwa shule ya Msingi Minazi Mirefu,iliyopo eneo la Kipawa Banana,Jijini Dar es Salaam leo.
Diwani wa Kata ya Kipawa,Mh. Boma Kaluwa akizungumza machache mbele ya mgeni rasmi,wageni waalikwa na Wanafunzi wa Shule hiyo wakati wa hafla hiyo fupi ya kukabidhi madawati 500 kwa shule ya Msingi Minazi Mirefu,iliyopo eneo la Kipawa Banana,Jijini Dar es Salaam leo.Mh. Kaluwa amekuwa akiwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kata yake inapata mafanikio makubwa hapa jijini kwa juhudi zake za kutafuta wafadhili mbali mbali ili waweze kumsaidia kuboresha maendeleo katika kata yake hiyo.

Mkurugenzi wa Mahusiano ya Serikari wa Kampuni ya African Barrick Gold, Emmanuel Ole-Naiko, akuzungumza  wakati wa hafla hiyo.

 Baadhi ya Walimu na Viongozi  wa Serikali ya mtaa wa Minazi Mirefu, wakiburudika kwa muziki wakati wakimkaribisha mgeni rasmi, ambaye ni Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,  Edward Lowassa (hayupo pichani).

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa, akiwapungia wanafunzi wa shule hiyo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa, akiwapungia wageni mbalimbali pamoja na wanafunzi wa shule hiyo.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa akisalimia na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Minazi Mirefu, iliyopo eneo la Kipawa Banana, Jijini Dar es Salaam leo wakiompokea kwa shangwe, alipofika shuleni hapo.

 Uongozi wa Kampuni ya African Barrick ukiwa katika picha ya mamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Minazi Mirefu, iliyopo eneo la Kipawa Banana, Jijini Dar es Salaam leo.

Wanafunzi wakibeba madawati.

No comments:

Post a Comment