TANGAZO


Tuesday, September 4, 2012

Lipumba atoa tamko mauaji ya mwandishi wa habari wa Chanel Ten, Daudi Mwangosi


Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akitoa tamko la chama chake kuhusu mauaji ya mwandishi wa habari wa kituo cha Tv cha Chane Ten, Daud Mwangosi, yaliyotokea Iringa Jumapili iliyopita. Kulia ni Naibu Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi wa chama hicho, Shaweji Mketo.


Waandishi wa habari wakimsikiliza na kunukuu maelezo ya tamko la Chama cha Wananchi (CUF), yaliyokuwa yakitolewa na Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba, Makao Makuu, Buguruni Dar es Salaam leo.

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akifafanua jambo kwa waandishi wakati alipokuwa akitoa tamko hilo leo.
 


Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akielezea jinsi tukio hilo la mauaji lisivyokubalika katika jamii iliyostaarabika na yenye amani. Kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF, Abdul Kambaya. 


Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, wakati alipokuwa akitoa tamko hilo, Makao Makuu, Buguruni Dar es Salaam leo.

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akisisitiza jambo, wakati alipokuwa akitoa tamko la chama chake kuhusu mauaji ya mwandishi wa habari wa kituo cha Tv cha Chane Ten, Daud Mwangosi, leo jijini. (Picha na Kassim Mbarouk)

BUGURUNI DAR ES SALAAM,
Septemba 4, 2012


Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amemtaka Rais Jakaya Kikwete kuunda tume huru kwa ajili ya kuchunguza mauji ya Mwangosi aliyefariki dunia Jumapili iliyopita mkoani Iringa.

Pia Prof. Lipumba amesema kwa sasa Jeshi la Polisi nchini haliwezi kukwepa lawama kutokana kifo cha Mwangosi kwani viongozi wa jeshi hilo wamekuwa na kauli ambazo zinatofautiana hali inayoonesha wazi tume huru itaweka wazi kila kitu kuhusu kifo cha mwandishi huyo. 

Akizungumza Dar es Salaam leo, Prof. Lipumba alisema wanalaani mauaji hayo na kwamba polisi wanapaswa kubeba lawama na si Chadema na kwamba lazima Rais aunde tume huru kuchunguza suala hilo.

"Kuna taarifa ambazo zinatofautiana katika tukio hili la kusikitisha, hivyo Watanzania wanataka kujua kifo chake na hiyo itawezekana kwa kuundwa tume huru ambayo itahusisha makundi mbalimbali na si vinginevyo,"alisema.

Alisema taarifa zilitolewa na vyombo vya habari pamoja na kunukuu polisi ni kuwa mwandishi huyo aliuawa kwa mlipuko akiwa mikononi mwa Jeshi la Polisi hadi kusababisha askari polisi waliokuwa karibu naye kujeruhiwa na mwingine kukimbizwa hospitali.

Prof. Lipumba alisema taarifa hizo zinatatanisha kwani zinasema mwandishi huyo alikimbilia kwa polisi kama kujisalimisha hadi  kukumbatiana na OCS aliyekuwepo  eneo hilo la tukio hilo. 

Lakini taarifa zaidi zinasema mwandishi huyo alikuwa amekwenda kumtetea mwandishi mwenzake wa vyombo vya IPP Media na askari aliyekuwa akimhami Mwangosi asiendelee kupata kipigo ndipo alipopigwa na mlipuko huo na kutawanya utumbo wake nje.

Prof. Lipumba alisema vurugu za kisiasa kati ya wafuasi wa Chadema  na Jeshi la Polisi si la kwanza ukiacha  lililotokea mkoani Arusha la kuuawa kwa watu watatu na tukio lingine la Agosti 27, mwaka huu mkoani Morogoro ambapo muuza magazeti, Ali Nzona anadaiwa kuuawa katika vurugu.

"Katika tukio la Morogoro polisi wanasema Nzona amefariki kwa kupigwa na kitu kizito kichwani wakati Chadema wanasema ameuawa baada ya kupigwa risasi,"alidai Prof. Lipumba. 


No comments:

Post a Comment