TANGAZO


Friday, September 14, 2012

Benki ya Posta yazindua Tovuti yake ya www.postalbank.co.tz

Mkurugenzi wa Kitengo cha IT wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Jema Msuya, azungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Tovuti ya benki hiyo, Dar es Salaam jana. Tovuti hiyo inapatikana kwa www.postalbank.co.tz. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Masoko, Andrew Chimazi. (Picha na Kassim Mbarouk)

 Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi (kulia), akiwa na baadhi ya waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari wakati wa uzinduzi wa tovuti hiyo, Dar es Salaam jana.

Baadhi ya Wakurugenzi na Maofisa wa benki ya Posta Tanzania (TPB), wakimsikiliza Mkurugenzi wa IT, Jema Msuya, wakati akizungumza kabla ya uzinduzi wa tovuti hiyo jijini jana.

 Baadhi ya waandishi wa habari wakiandika maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mkurugenzi wa IT, Jema Msuya (hayupo pichani), wakati akizungumza kabla ya uzinduzi wa tovuti hiyo jijini jana.

Mkurugenzi wa Kitengo cha IT wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Jema Msuya, akiwaelezea waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, ni kwa nini hasa kilichopelekea kuanzishwa kwa Tovuti hiyo.

Mkurugenzi wa Kitengo cha IT wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Jema Msuya, akiielezea tovuti hiyo muundo wake pamoja na mambo mbalimbali yaliyomo kwenye tovuti, ikiwemo pia matangazo ya nafasi za kazi, historia, huduma mbalimbali zitolewazo na benki hiyo pamoja na taarifa mbalimbali kuhusiana na benki ya TPB.

Meneja Mwandamizi wa Mawasiliano na Uhusiano, Noves Moses akielezea jambo kwa waandishi wa habari, wakati wa uzinduziwa tovuti hiyo.

Waandishi wa habari wakijadili jambo, wakati wa uzinduzi wa tovuti hiyo.

Mkurugenzi wa Kitengo cha IT wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Jema Msuya, akielezea kuhusu mambo muhimu waliyoyazingatia kwenye tovuti hiyo kwa waandishi wa habari wakati wa uzinduzi jana.

Mkurugenzi wa Kitengo cha IT wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Jema Msuya, akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari, wakati waandishi hao, walipotaka kujua masuala kadhaa kuhusiana na tovuti hiyo.

Meneja Mwandamizi wa Mawasiliano na Uhusiano, Noves Moses (kulia), akiwa na mmoja wa wataalamu wa tovuti hiyo, Aliasgar Tayabali, wakiangalia muundo wa tovuti hiyo.

Mmoja wa waandishi wa habari, akitaka ufafanuzi kuhusu mahusiano ya tovuti hiyo na wateja wa benki hiyo pamoja na wananchi wengine, hasa wa vijijini katika kupata huduma za benki hiyo.
 
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, wakati wa uzinduzi wa tovuti hiyo jana.

Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi (kulia), akiizindua tovuti ya www.postalbank.co.tz Makao Makuu ya benki hiyo, Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kitengo cha IT wa benki hiyo, Jema Msuya.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi (kulia) na Mkurugenzi wa Kitengo cha IT wa benki hiyo, Jema Msuya (kushoto), wakifurahi na kupiga makofi, wakati Mkurugenzi huyo, Mkuu, alipoizindua tovuti hiyo ya www.postalbank.co.tz, Makao Makuu ya benki hiyo, Dar es Salaam jana.
 

Maofisa wa benki ya Posta Tanzania (TPB), Chichi Banda (kushoto) na Cristina Mselewa, wakifurahia uzinduzi huo.

No comments:

Post a Comment