TANGAZO


Monday, August 6, 2012

Yanga watinga Bungeni mjini Dodoma na Kombe la Kagame

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga wa pili kulia, akiwa na kocha Mkuu wa timu hiyo, Tom Saintfiet, wakati walipofika kwenye ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma leo kwa ajili ya kuwaonesha Wabunge kombe waliloshinda katika mashindano ya Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup), hivi karibuni.
Baadhi ya wachezaji na viongozi wa Yanga wakiwa ndani ya ukumbi wa Bungeni mjini Dodoma leo.


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (wa nne kushoto waliosimama mstari wa mbele), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wachezaji wa timu ya Yanga, ambao walilipeleka Kombe la Ubingwa wa michuano ya Kombe la Kagame Bungeni, mjini Dodoma leo. Kushoto kwake ni Mlezi na mdhamini wa Klabu hiyo, Mama Fatuma Karume. (Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment