TANGAZO


Thursday, August 2, 2012

Rais Shein awaandalia futari wananchi wa Kusini Pemba, amaliza ziara kisiwani Pemba

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, (kushoto), akisalimiana na viongozi na wananchi wa Mkoa wa Kusini Pemba, alipowasili katika viwanja vya Shule ya Mkanyageni Pemba, wakati wa chakula cha Futari alichowaandalia wananchi na waumini wa kijiji cha Mkanyageni kisiwani humo 
jana. (Picha zote na Ramadhan Othman, Ikulu)

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia), akijumuika na  wananchi wa kijiji cha Mkanyageni Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba, wakati wa chakula cha Futari, alichowaandalia  wananchi hao katika viwanja vya Shule ya Mkanyageni  jana.

Baadhi ya akina mama wa kijiji cha Mkanyageni, Mkoa wa Kusini Pemba wakijitayarisha kwa ajili ya chakula cha Futari kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, viwanja vya Shule ya Mkanyageni Pemba jana.

Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mama Mwanamwema Shein (katikati), akijumuika na  akinamama wa kijiji cha Mkanyageni, Mkoa wa Kusini Pemba katika  Chakula cha Futari kilichoandaliwa kwa wananchi hao na Rais wa Zanzibar, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, viwanja vya Shule ya Mkanyageni Wilaya ya Mkoani, kisiwani Pemba  jana.

Baadhi ya wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu wa kijiji cha Mkanyageni Mkoa wa Kusini Pemba, wakiwa katika  chakula cha Futari kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein katika viwanja vya Shule ya Mkanyageni, kisiwani Pemba jana.

Sheikh Yussuf Abdalla wa kijiji cha Mkanyageni, Wilaya ya Mkoani Pemba, akitoa shukurani kwa niaba ya wananchi wa kijiji hicho kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein kwa kuwaandalia Chakula cha Futari, kilichofanyika jana katika Viwanja vya Shule ya Mkanyageni Mkoa wa Kusini Pemba.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto), akiagana na wananchi wa kijiji cha Mkanyageni, Mkoa wa Kusini Pemba jana, baada ya Chakula cha Futari alichowaandalia katika viwanja vya Shule ya Mkanyageni.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Ahaj Dk. Ali Mohamed Shein na mkewe mama Mwanamwema Shein, wakiagana na viongozi wa Mikoa ya Pemba katika Uwanja wa Ndege wa Karume Pemba, baada ya kumaliza ziara ya kisiwani humo leo.

No comments:

Post a Comment