Mrisho Ngassa akiingia Makao Makuu ya Klabu ya Simba, mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutambulishwa rasmi leo.
Mashabiki wa Simba, wakimpokea Ngassa kwa shangwe, alipokuwa akiwasili Klabu ya Simba, mtaa wa Msimbazi na Agrey jijini leo. |
Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu', akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kumtambulisha rasmi mshambuliaji wa timu hiyo, Mrisho Khalfan Ngassa, Makao Makuu ya klabu hiyo leo, Msimbazi jijini Dar es Salaam leo.
Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu', akimkabidhi jezi namba 16 ya timu hiyo, aliyekuwa mshambuliaji wa Azam FC, Mrisho Khalfan Ngassa, baada ya kujiunga rasmi na Wekundu hao wa Msimbazi kwa mkataba wa miaka miwili.
Ngassa akipokea jezi namba 16 kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Simba, Godfrey Nyange 'Kaburu' leo. |
Mshambuliaji mpya wa Simba, Mrisho Ngassa akivaa jezi ya Simba baada kujiunga na timu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Azam FC.
Ngassa akionesha namba ya jezi yake, mara baada ya kukabidhiwa na Makamu Mwenyekiti wa timu hiyo, Godfrey Nyange 'Kaburu' leo. |
Mrisho Ngassa akifuhia jezi ya Simba baada ya kuvaa.
Gari alilopewa Mrisho Ngassa baada ya kujiunga na Simba leo.
Mshambuliaji mpya wa Simba, Mrisho Ngassa akiwa na wachezaji wenzake kwenye mazoezi yaliyofanyika katika ufukwe wa Coco Beach leo.
Mshambuliaji mpya wa Simba, Mrisho Ngassa akizungumza jambo na Nahodha wa Simba, Juma Kaseja wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika ufukwe wa Coco Beach leo. |
Mrisho Ngasa akifanya mazoezi na timu yake mpya ya Simba leo, Coco Beach.
Ngassa nyuma ya Mwinyi Kazimoto, akiwa mazoezini Coco Beach leo asubuhi. |
Mrisho Ngassa akipiga mpira na Amri Kiemba katika mazoezi hayo leo.
Ngassa akifanya mazoezi ya kunyoosha viungo.
Mrisho Ngasa akizungumza jambo na Uhuru Suleiman baada ya kumaliza mazoezi kwenye ufukwe wa Coco Beach leo asubuhi.
Mshambuliaji mpya wa Simba Mrisho Ngasa akiwa ndani ya gari lake, baada ya kumalizika kwa mazoezi ya timu hiyo, kwenye fukwe za Coco Beach leo asubuhi.
Ngassa ndani ya mchuma wake mpya aliokabidhiwa na timu yake mpya ya Simba leo. (Picha zote na Picha zote na Habari Mseto Blog)
No comments:
Post a Comment