Mratibu wa Tamasha la Injili la Pasaka Tanzania, Alex Msama wa Msama Promosion (kushoto), akimkabidhi msaada wa sh. mil. 1, mchezaji wa zamani wa Simba na Taifa Stars, Alphonce Modest kwa ajili ya kusaidia matibabu ya miguu inayosumbua na baridi yabisi. Msaada huo uliokabidhiwa Dar es Salaam leo, ulihamasishwa na Mhariri Kiongozi wa gazeti la Champion, Saleh Ali (wa pili kushoto), pamoja na mtangazaji wa kituo cha Televisheni cha Channel Ten na Radio Magic FM, Said Kilumanga (wa pili kulia). Wahamasishaji hao, wameiomba jamii yenye huruma, kumsaidia kwa hali na mali mchezaji huyo, ambaye wamemsafirisha kwa gharama zao kutoka Mwanza. (Picha zote na Richard Mwaikenda)
Alphonce Modest akitembea kwa taabu huku akisaidiwa na mdogo wake Francis. |
Alphonce Modest, anavyoonekana kwa sasa. |
Alphonce Modest akitoa shukrani kwa Msama na kuelezea jinsi ugonjwa huo ulivyompata na kumsababishia kulazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando, jijini Mwanza kwa mwaka mzima wa 2011. |
No comments:
Post a Comment