TANGAZO


Monday, August 6, 2012

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Kone atembelea Wizara ya Fedha Maonesho ya Nanenane mjini Dodoma

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone (kushoto), akitaka kujua  maoni kutoka kwa   Mhasibu wa Wizara ya Fedha Abbas Myeto(kulia), kuhusu taratibu za kupata pesheni kwa watumishi wa umma wanapostaafu. Mkuu huyo wa Mkoa wa Singida aliomba ufafanuzi huo jana, alipotembelea banda la Wizara ya Fedha katika maonesho ya Wakulima Kitaifa ya Nanenane yanayoendelea mjini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone (kushoto) akipata maelezo mafupi  jinsi  Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA), inavyosaidia katika kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma, yaliyokuwa yakifanyika kupitia ununuzi wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya Ofisi za Serikali na taasisi zake. Mkuu huyo wa Mkoa, alipata maelezo hayo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Menejimenti ya Mikataba Maalum Modecai Mato (kulia) jana, alipotembelea banda la Wizara ya fedha katika maonesho ya Wakulima Kitaifa ya Nanenane yanayoendelea mjini Dodoma.

Mchambuzi wa Mifumo ya Kompyuta Mkuu, Daraja la III kutoka Idara ya Menejimenti ya TEKNOHAMA ya Kifedha, Wizara ya Fedha, Margeth Ambrosi Nembo (kushoto), akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk.  Parseko Kone jana mjini Dodoma, jinsi ya kuingiza mishahara na malimbikizo ya watumishi wa umma kwa kutumia TEKNOHAMA . Mkuu huyo Mkoa, alikuwa katika maonyesho ya Wakulima Nanenane mjini Dodoma.

Meneja Mawasiliano na Kumbukumbu wa Shirika Hodhi la Mali ya Mashirika ya Umma (CHC), Joseph Mapunda (kushoto), akimpa  Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk.  Parseko Kone (kulia) jana, jinsi Shirika hilo, linavyofanya tathmini ya mashirika ya umma yaliyobinafsishwa na utendaji wa mashirika hayo, wakati alipotembelea banda la Wizara ya Fedha katika maonyesho ya Wakulima ya Nanenane mjini Dodoma.

Ofisa Uhusiano na Masoko wa Chuo cha Mipango Dodoma, Godrick Ngoli (kulia), akimpa maelezo Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone (kushoto) jana, jinsi Chuo hicho kinavyotarajia kutoa kozi mbalimbali zinahusu mazingira ili kukabiliana na changanoto ya ongezeko la watu nchini. Mkuu huyo wa Mkoa alipata maelezo hayo wakati alipotembelea banda la Wizara ya Fedha katika maonyesho ya Wakulima Nanenane mjini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone (kushoto), akitoa changamoto kwa watumishi wa Chuo cha Mipango cha Dodoma kuwa na mitaala ambayo itawaandaa wananchi kuanzia ngazi ya chini juu ya kuwa na mipango mizuri ya matumzi bora ya ardhi ili kukabiliana na ongezeko la watu nchini. Mkuu Mkoa huyo alitoa kauli hiyo jana mjini Dodoma alipotembelea banda la Wizara ya Fedha katika maonyesho ya Wakulima Nanenane mjini Dodoma. (Picha zote na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dodoma)

No comments:

Post a Comment