Mkuu wa kitengo cha Menejimenti ya Mikataba kutoka Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA), Mordecai Matto (kulia), akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (kushoto), leo mjini Dodoma juu ya kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma wakati alipotembelea banda la Hazina kwenye maonesho ya Nanenane, mjini humo. (Picha zote kwa hisani ya Hazina)
Mkuu wa kitengo cha Menejimenti ya Mikataba kutoka Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA), Mordecai Matto (kulia), akitoa ufafanuzi kwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue(kushoto), leo mjini Dodoma juu ya kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma wakati Katibu Kiongozi, alipotembelea banda la Wizara ya Fedha kwenye maonesho hayo.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (wa pili kulia), akisamiliana na watumishi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Mchambuzi wa Mifumo ya Kompyuta Ibrahim Sultan (wa pili kushoto) na Afisa Taalum Mwandamizi Mkiramwene Msafiri(kushoto), leo mjini Dodoma, alipotembelea banda la Wizara ya Fedha kwenye maonesho ya wakulima ya nanenane mjini humo.
Mchumi Mwandamizi wa Idara ya Bajeti, Wizara ya Fedha, Adam Msumule ( wa pili kushoto), akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (kulia), jinsi wanavyoelimisha wananchi juu ya uchambuzi wa bajeti kwa njia rahisa ili waweze kujua mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka husika wa fedha leo, wakati Katibu Mkuu Kiongozi, alipotembelea banda la Wizara ya Fedha kwenye maonesho ya Wakulima ya Nanenane mjini Dodoma.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, akisaini kitabu cha wageni leo, mjini Dodoma, alipotembelea banda la Wizara ya Fedha kwenye maonesho ya Wakulima ya Nanenane mjini Dodoma, kuona shughuli mbalimbali za Wizara hiyo katika maonesho hayo. Kushoto ni Ofisa wa Wizara ya Fedha, Ramadhan Omary. (Picha zote na Hazina)
No comments:
Post a Comment