Balozi wa Switzerland nchini, Olivier Chave, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu maonesho 3 ya mwanamuziki wa Kimataifa wa muziki wa jazz, Malcolm Braff (katikati), atakayofanya nchini kwa kushirikiana na wasanii wa Tanzania. Kulia ni mmoja wa wasanii hao, Paul Nduguru wa kundi la Wahapa hapa. (Picha zote na Kassim Mbarouk)
Mwanamuziki wa Kimataifa wa muziki wa jazz, Malcolm Braff (katikati), akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu maonesho matatu atakayofanya nchini kwa kushirikiana na wasanii wa Tanzania. Kushoto ni Balozi wa Switzerland nchini, Olivier Chave na kulia ni mmoja wa wasanii hao, Paul Nduguru wa kundi la Wahapa hapa.
Mmoja wa wasanii wakatakaoshirikiana na mwanamuziki wa Kimataifa wa muziki wa Jazz kutoka Switzerland, Malcolm Braff (katikati), Paul Nduguru wa kundi la Wahapa hapa, akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano huo. Kushoto ni Balozi wa Switzerland nchini, Olivier Chave.
Mmoja wa wasanii wakatakaoshirikiana na mwanamuziki wa Kimataifa wa muziki wa Jazz kutoka Switzerland, Malcolm Braff (kulia), katika kutumbuiza kwenye maonesho yake nchini, Kelvin Erasmus wa kundi la Wakwetu, akizungumza katika mkutano huo leo. Katikati ni Balozi wa Switzerland nchini, Olivier Chave.
Baadhi ya waandishi wa habari, waliokuwa wakifuatilia mazungumzo hayo, wakinukuu maelezo mbalimbali, yaliyokuwa yakitolewa kwenye mkutano huo, ukumbi wa Idara ya Habari, Maelezo jijini Dar es Salaam leo.
Mwanamuziki wa Kimataifa wa muziki wa jazz, Malcolm Braff, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano huo, Dar es Salaam leo, kuelezea kuhusu maonesho yake matatu atakayofanya nchini kwa kushirikiana na wasanii wa Tanzania. Kushoto ni Balozi wa Switzerland nchini, Olivier Chave.
Mratibu wa maonesho hayo, Kwame Mchauru (kushoto), akifafanua jambo kuhusu maonesho hayo, wakati wa mkutano huo leo, Idara ya Habari, Maelezo jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment