TANGAZO


Saturday, August 4, 2012

Azaki wilayani Mkuranga zapitisha rasimu ya Katiba ya umoja wao, zafanya uchaguzi

Ofisa Tarafa wa Wilaya ya Mkuranga, Yassin Majuto, akizungumza na wajumbe wa mkutano wa Mitandano ya Asasi zisizo za Kiserikali (Azaki), wilayani Mkuranga leo, wakati alipokuwa akiufungua mkutano wao wa kujadili na kupitisha rasimu ya Katiba na uchaguzi wa viongozi wa mtandao wa Mkoa Pwani. Kushoto ni Mratibu wa Asisi zisizo za Kiserikali, Ibrahim Salim na kulia ni Mratibu wa Mtandao wa Asasi hizo, Mohamed Katundu. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa Mitandao ya Asasi zisizo za Kiserikali (Azaki), Wilaya za Mkoa wa Pwani wakiwa  katika mkutano wao wa kujadili na kupitisha rasimu ya Katiba na uchaguzi wa viongozi wa watakauongoza umoja huo, leo wilayani humo, wakimsikiliza mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano huo, Ofisa Tarafa wa Wilaya ya Mkuranga, Yassin Majuto.

Wajumbe wa mkutano wa Mitandao ya Asasi zisizo za Kiserikali (Azaki) za Wilaya za Mkoa wa Pwani, wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufunguliwa  kwa  mkutano wao wa kujadili na kupitisha rasimu ya Katiba na uchaguzi wa viongozi watakauongoza umoja wao, wilayani humo leo.


Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wa Mitandao ya Azaki ya Wilaya za Mkoa wa Pwani, wakiwa katika picha ya pamoja, mara baada ya kufunguliwa kwa mkutano huo na Ofisa Tarafa wa Wilaya ya Mkuranga, Yassin Majuto (hayupo pichani), leo wilayani humo.


Waratibu wa Mitandao ya Asasi zisizo za Kiserikali (Azaki), Wilaya za Mkoa wa Pwani, wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufunguliwa kwa mkutano wa Asasi hizo na Ofisa Tarafa wa Wilaya ya Mkuranga, Yassin Majuto (hayupo pichani) leo.

Waratibu wa Mitandao ya Asasi zisizo za Kiserikali (Azaki), za Wilaya za Mkoa wa Pwani, wakiwa na Maofisa wa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Mkuranga katika picha ya pamoja mara baada ya kufunguliwa kwa mkutano wa Asasi hizo, wilayani humo na Ofisa Tarafa wa Wilaya hiyo, Yassin Majuto (hayupo pichani) leo.

Wahazini wa Mitandao ya Asasi zisizo za Kiserikali (Azaki) za Mkoa wa Pwani, wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufunguliwa kwa mkutano wa Asasi hizo na Ofisa Tarafa wa Wilaya hiyo, Yassin Majuto (hayupo pichani) leo.


Mratibu wa Asisi zisizo za Kiserikali, Ibrahim Salim, akizungumza katika mkutano huo, mara baada ya kuzinduliwa na Ofisa Tarafa wa Wilaya ya Mkuranga, Yassin Majuto (hayupo pichani) leo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Citizen Parliamentary Watch, Marcusy Alban.


Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa Asasi zisizo za Kiserikali (Azaki), wilayani Mkuranga wakisikiliza masuala mbalimbali yaliyokuwa yakijadiliwa kwenye mkutano wao.

Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Citizen Parliamentary Watch, Marcusy Alban, akizungumza kwenye mkutano huo, wakati alipokuwa akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali.

No comments:

Post a Comment