Kikosi cha timu ya Azam FC, kilichopambana na Yanga African katika mchezo wa Fainali wa Kombe la Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup), Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni. (Picha zote na Kassim Mbarouk)
Kikosi cha Yanga African, kilichopambana na Azam FC katika mchezo wa fainali wa Kombe la Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup), Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni.
Mchezaji Ibrahim Mwaipopo wa Azam (katikati), akiwania mpira na Athuman Idd (kushoto) na Rashid Gumbo, wote wa Yanga katika fainali hiyo.
Mchezaji Stephano Mwasika wa Yanga, akiupiga kichwa mpira, kuuondoa katika hatari huku akiangaliwa na Kipre Tchetche (kulia) wa Azam na Nadir Haroub 'Canavaro' (kushoto) wa Yanga.
Mchezaji Kipre Tchetche wa Azam FC, akiudhibiti mpira katika mchezo huo.
John Boko wa Azam FC (katikati), akitafuta mbinu ya kumtoka Nadir Haroub wa Yanga, huku Ibrahim Mwaipopo (nyuma) wa timu hiyo, akimuangalia.
John Boko wa Azam FC, akimtoka Nadir Haroub 'Canavaro' wa Yanga katika kipute hicho.
Mchezaji George Odhiambo (kushoto) wa Azam FC, akijaribu kumpiga chenga Oscar Joshua wa Yanga.
John Boko wa Azam FC (katikati), akitafuta mbinu ya kuwatoka Shamte Ali (kushoto) na Rashid Gumbo, wote wa Yanga.
Mashabiki wa Yanga, wakifuatilia kwa makini, mchezo huo, uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni.
Mashabiki wa Azam FC, wakiangalia kwa huzuni mchezo huo, baada ya timu yao kutundikwa bao la kwanza katika dakika za nyongeza za kipindi cha kwanza za kipute hicho, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao la pili la timu hiyo, lililowahakikishia ushindi na ubingwa wa kombe hilo, bao lililofungwa na Said Bahanuzi katika dakika za lala salama, uwanjani hapo.
Hadi mwisho wa mchezo, ubao wa matangazo ulikuwa ukionesha Yanga - 2 na Azam FC - 0.
Makocha wa Azam FC, Stewart Hall (kushoto) na Tom Saintfiet wa Yanga wakijadili jambo kuhusu mchezo huo, wakati mchezo ulipomalizika uwanjani hapo leo jioni, Yanga wakiwa washindi wa mabao 2-0 na hivyo kukabidhiwa kombe la ubingwa huo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadik.
Mchezaji Hamis Kiiza wa Yanga, akiwapongeza wanachama na mashabiki wa timu hiyo, baada ya kumalizika mchezo huo.
Mashabiki wa Yanga wakishangilia kwa kuwasha fashifashi, uwanjani hapo.
Mjumbe wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Crisent Magori, akimvisha medali mwamuzi wa mchezo huo, Thiery Nkurunziza wa Burundi. Kulia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu, Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholus Musonye.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadik, akiwavisha medali za dhahabu wachezaji wa Yanga, wakati wa kukabidhi zawadi na kombe la ubingwa huo, uwanjani hapo leo jioni.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadik (katikati), akilinyanyua juu Kombe la Ubingwa huo, kumkabidhi Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub 'Canavaro' (kushoto), mara baada ya kuwavisha medali wachezaji hao.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia kombe la ubingwa huo, mara baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadik, uwanjani hapo.
No comments:
Post a Comment