Mkuu wa Kitengo cha Wagonjwa wa Dharura wa Hospitali ya Amana, Christopher Mzava, akizungumza na waandishi wa habari hospitali hapo leo, kuhusu wananchi, wakazi wa Kigogo, waliokunywa pombe aina ya gongo na baadhi yao, wanne kupoteza maisha jana na leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk)
Mmoja wa wananchi waliodhurika kwa kunywa pombe hiyo haramu, aina ya gongo, Raphael Expendito, akiwa Hospitali ya Amana akipatiwa matibabu leo.
Mwananchi aliyedhurika kwa kunywa pombe haramu, aina ya gongo, Raphael Expendito, akizungumza na waandishi wa habari kwenye Hospitali ya Amana leo, wakati akipatiwa matibabu.
Mmoja wa waathirika wa pombe hiyo, akizungumza na waandishi wa habari kwenye wodi ya hospitali ya Amana, jijini Dar es Salaam leo, alikokuwa akitibiwa.
No comments:
Post a Comment