TANGAZO


Thursday, July 12, 2012

TEA kuzindua kampeni ya ujenzi wa hosteli za wanafunzi wa kike wa Shule za Sekondari nchini

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Esther Abayo, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusu uzinduzi wa kampeni maalum kwa ajili ya ujenzi wa hosteli za wanafunzi wa kike katika Shule za Sekondari nchini utakaofanyika tarehe 14 Julai 2012, Kibaigwa mkoani Dodoma. Kushoto ni Meneja Habari Elimu na Mawasiliano, Sylvia Lupembe. 
 
 Meneja Habari Elimu na Mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Sylvia Lupembe akifafanua jambo kwa waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati uongozi wa mamlaka hiyo, ulipozungumza nao kuhusu uzinduzi wa kampeni maalum kwa ajili ya ujenzi wa hosteli za wanafunzi wa kike katika Shule za Sekondari nchini, utakaofanyika tarehe 14 Julai Kibaigwa mkoani Dodoma. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Esther Abayo na Mkurugenzi wa Uhamasishaji Rasilimali Watu, Seif Mohamed.
 
Mkurugenzi wa Uhamasishaji Rasilimali Watu, Seif Mohamed akifafanua jambo kuhusu  uzinduzi wa kampeni maalum kwa ajili ya ujenzi wa hosteli za wanafunzi wa kike katika Shule za Sekondari nchini, utakaofanyika tarehe 14 Julai, 2012, Kibaigwa mkoani Dodoma. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Esther Abayo. (Picha zote na Francis Dande)

No comments:

Post a Comment