Rais
Jakaya Mrisho kikwete, Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda na mkewe
Mama Janet Museveni, Waziri Mdogo wa Uingereza wa Maendeleo ya Kimataifa, Stephen O'Brien (kulia) na Mama Melinda Gates wakibadilishana
mawazo kabla ya kuhutubia katika mkutano wa kimataifa wa viongozi,
kujadili Uzazi wa Mpango kwa nchi masikini zaidi duniani katika ukumbi
wa Queen Elizabeth II, jijini London July 11, 2012. Mkutano huo ni wa
kwanza wa aina yake duniani na umeanzisha mchakato wa dunia ambao
utalenga kuwawezesha wanawake wapatao milioni 120 katika nchi masikini
zaidi duniani kupata habari, huduma na mahitaji ya kupanga uzazi bora
zaidi na kuokoa maisha yao ifikapo mwaka 2020.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akuhutubia katika mkutano wa kimataifa wa
viongozi kujadili Uzazi wa Mpango kwa nchi masikini zaidi duniani,
katika ukumbi wa Queen Elizabeth II, jijini London July 11, 2012. Mkutano
huo ni wa kwanza wa aina yake duniani na umeanzisha Mchakato wa Dunia
ambao utalenga kuwawezesha wanawake wapatao milioni 120 katika nchi
masikini zaidi duniani kupata habari, huduma na mahitaji ya kupanga
uzazi bora zaidi na kuokoa maisha yao ifikapo mwaka 2020.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri Mkuu wa Uingereza, Donald
Cameron, Rais Paul Kagame wa Rwanda na Rais Yoweri Kaguta Museveni wa
Uganda wakijiandaa kupanda jukwaani kuhutubia katika mkutano wa
kimataifa wa viongozi, kujadili Uzazi wa Mpango kwa nchi masikini zaidi
duniani, katika ukumbi wa Queen Elizabeth II, jijini London July 11,
2012.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete (wa tatu kushoto) na ujumbe wake, wakiwa katika mazungumzo na Afisa
Mtendaji Mkuu wa British Gas (BG Group), Sir Frank Chapman (wa pili
kulia) na maofisa waandamizi wa kampuni hiyo. BG Group imewekeza kiasi
cha Pauni milioni 80 za Uingereza (Shilingi Trilioni 125) katika mradi wa
kuchimba gesi asilia nchini Tanzania, na tayari visima vitano vya
nishati hiyo vimeshatema gesi nyingi katika bahari kuu kusini mwa
Tanzania maeneo ya Mtwara. Hii ilikuwa ni ziara fupi katika Makao Makuu
ya BG Group mjini Reading, Uingereza ambako Rais Kikwete na ujumbe wake
walitembelea Julai 11 kujionea namna kazi za uvumbuzi wa gesi asilia
unavyofanywa na kampuni hiyo, yenye kufanya shughuli zake katika nchi 21
katika mabara matano, ikiwa na jumla ya wafanyakazi 6,000.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Afisa Mtendaji Mkuu wa British Gas
(BG Group), Sir Frank Chapman alipotembelea Makao Makuu ya Kampuni hiyo,
mjini Reading Uingereza Julai 11, 2012. BG Group imewekeza kiasi cha
Pauni milioni 80 za Uingereza (Shilingi Trilioni 125) katika mradi wa kuchimba
gesi asilia nchini Tanzania na tayari visima vitano vya nishati hiyo
vimeshatema gesi nyingi katika bahari kuu kusini mwa Tanzania maeneo ya
Mtwara.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete (wa pili kulia) na ujumbe wake, wakipata maelezo ya maendeleo ya
uchimbaji wa gesi asilia nchini Tanzania, walipotembelea Makao Makuu ya
British Gas (BG Group), ambayo imewekeza kiasi cha Pauni milioni 80 za Uingereza
(Shilingi Trilioni 125) katika mradi wa kuchimba gesi asilia nchini
Tanzania.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Waziri Mdogo
wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza, Stephen O'Brien jijini
London jana, ambapo Uingereza iliahidi kuendelea kuisaidia Tanzania katika
mambo mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kusaidia kuendeleza
sekta ya nishati hususan utafutaji wa gesi asilia.
Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi akiongea na baadhi ya
wajumbe wa mkutano wa kimataifa wa Uzazi wa Mpango katika ukumbi wa
Queen Elizabeth II, jijini London Julai 11, 2012. Kushoto ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Chama cha Uzazi na Malezi Bora Tanzania (UMATI), Josephine Mwankusye na kulia ni Naibu Mkurugenzi wa Afya ya Mzazi na
Mtoto katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Neema Rusibamayila. (Picha zote na Ikulu)
No comments:
Post a Comment