TANGAZO


Sunday, July 29, 2012

Tanzania yalala 2-1 mbele ya Nigeria mashindano ya U 20

Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania ya Vijana chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes, Frank Domayo akijaribu kumtoka beki wa Flying Eagles, Ahiyu Mohammed katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Nigeria imeshinda 2-0. 

 Mshabuliaji wa timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 20, Ramadhani Singano (kulia), akichuana na beki wa Flying Eagles, Ahiyu Mohammed  katika mechi ya kwanza ya raundi ya pili katika kampeni ya kuwania tiketi ya kucheza fainali za Afrika nchini Algeria 2013. 

Wachezaji wa akiba wa timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 20 ya Nigeria, Flying Eagles wakishangilia baada ya timu yao kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo huo.  (Picha zote na habari Mseto Blog)

No comments:

Post a Comment