TANGAZO


Monday, June 18, 2012

Wakufunzi wa Sensa wapigwa msasa mjini Dodoma



Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi  ya Taifa ya Takwimu, Dk. Albina Chuwa, akitoa ufafanuzi kwa wakufunzi wa Sensa  kwa ngazi ya Kitaifa  jana mjini Dodoma. Wakufunzi  hao wanaandaliwa kwa ajili ya kwenda katika Mikoa mbalimbali nchini kwa ajili ya kuwaelimisha wengine watakaosaidia kufanikisha zoezi la sensa Agosti 26 mwaka huu. (Picha zote na Vicent Tiganya wa MAELEZO)
Baadhi ya viongozi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu na wakufunzi wa Sensa kwa ngazi ya Kitaifa wakiwa wametulia kimya kwa dakika mbili kwa ajili ya kuombeleza kifo cha Mhariri wa Gazeti la Jamboleo, Willy Edward kilichotokea mjini Morogoro alipokuwa akihudhuria mafunzo ya sense kwa wahariri. Viongozi na wakufunzi hao walikuwa katika mafunzo  ya siku 10, tayari kwa ajili ya kwenda kufundisha hatua za Mikoa. Mafunzo hayo yanaendeshwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na kualianza jana mjini Dodoma.
Kamishna wa Sensa nchini, Hajjat Amina Mrisho, akitoa neno la utangulizi kwa  wakufunzi wa Sensa kwa ngazi ya Kitaifa, wakati wa  mafunzo  ya siku 10, tayari kwa ajili ya kwenda kufundisha hatua za Mikoa. Mafunzo hayo yanaendeshwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), mjini Dodoma.
Baadhi ya wakufunzi wa Sensa kwa ngazi ya Kitaifa, wakiwa katika mafunzo  ya siku 10, kwa ajili ya kwenda kufundisha hatua za mikoa, wakifuatilia mafunzo kutoka kwa wataalamu mbalimbali waliokuwa wakitoa mada mbalimbali. Mafunzo hayo yanaendeshwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na yameanza jana mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment