Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa benki ya UBA, Imo Etuk, akiwasalimia yatima wa kituo cha New Hope Family for Street Children Centre, kilichopo Kigamboni, jijini wakati wafanyakazi wa benki hiyo, walipowatembelea vijana hao kwa ajili ya kujumuika nao na kuwapa misaada ya vyakula mbalimbali.
Wafanyakazi wa benki ya UBA wakipata kifungua kinywa na watoto wa New Hope Family for Street Children Centre, kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam, wilayani Temeke, mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi Mkuu wa benki ya UBA Tanzania, Daniel Addo, Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa UBA, Imo Etuk na Meneja Rasilimali Watu wa benki hiyo, Daniel Mkenda (wote kushoto), wakikabidhi mafuta ya kula kwa mmoja wa yatima hao, ikiwa ni moja ya misaada mbalimbali ya vyakula walitowa msaada kwa watoto wa kituo hicho mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi Mkuu wa benki ya UBA Tanzania, Daniel Addo, Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa UBA, Imo Etuk na Meneja Rasilimali Watu wa benki hiyo, Daniel Mkenda (wote kushoto), wakikabidhi sabuni na mafuta ya kula kwa walezi wa kituo hicho, ikiwa ni kati ya misaada mbalimbali ya vyakula na vitu vingine kwa ajili ya matumizi ya yatima wa kituo hicho.
Wafanyakazi wa benki ya UBA, wakiwa pamoja na yatima wa kituo cha New Hope Family for Street Children Centre, Kigamboni wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam, wakiimba na kufurahia pamoja, mwishoni mwa wiki, walipowatembelea kwa ajili ya kujumuika nao na kutoa misaada mbalimbali, ikiwemo ya vyakula na vitu vinginevyo.
Wafanyakazi wa United Bank for Africa wakifanya mazoezi ya viuongo baada ya kufanya jogging ya umbali wa kilometa tano, kutoka Kivukoni mpaka Kijiji Beach.
Resort Kigamboni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Wafanyakazi wa benki ya UBA wakicheza mchezo wa mpira wa wavu, Kijiji Beach Resort Kigamboni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. (Picha zote na mpigapicha wetu) |
No comments:
Post a Comment