TANGAZO


Monday, June 18, 2012

Deloitte, yaandaa semina juu ya Bejeti za nchi za Afrika ya Mashariki 2012/13, Dar es Salaam


Meneja Mkuu wa taasisi inayojishughulisha na mambo ya uchumi ya Deloitte Tanzania, Yanaz Mngumi, akiwasilisha mada kuhusu mabadiliko ya kodi ya Tanzania wakati wa semina ya kujadili bajeti za nchi za Afrika ya Mashariki kwa mwaka 2012/13, Dar es Salaam leo jioni, hoteli ya Serena. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

Baadhi ya washiriki wa semina hiyo, wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye semina hiyo.

 Washiriki wa semina ya kujadili bajeti za nchi za Afrika ya Mashariki, iliyotayarishwa na taasisi ya mambo ya uchumi ya Deloitte, wakisiliza mada zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye semina hiyo leo jioni.

Meneja wa Deloitte nchini, Denis Kakembo, akiwasilisha mada kuhusu mtazamo wa jumla wa bajeti za Kenya na Uganda wakati wa semina hiyo jioni hii.

 Washiriki wakisikiliza na kufuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika semina hiyo ya Deloitte East Africa 2012/13, Bugdet jijini Dar es Salaam leo.

Mkurugenzi wa Deloitte, Bill Page, akitoa uchambuzi juu ya hali ya uchumi wa nchi za Afrika ya Mashariki baada ya kutangazwa kwa bajeti za nchi hizo juzi.

Mkurugenzi wa taasisi inayojishughulisa na mambo ya uchumi ya Deloitte, Bill Page akifafanua jambo kuhusu bajeti hizo, kwa wanasemina hiyo ya Deloitte East Africa 2012/13 Bugdet Seminar jijini jioni hii. Wengine ni wachambuzi wa masuala ya uchumi nchini.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda nchini, Felix Mosha, akifafanua kuhusu uchumi wa nchi za Afrika ya Mashariki utakavyokuwa baada ya kusomwa bajeti za nchi hizo na kutoa tathmini ya jumla kwa nchi hizi. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa taasisi ya The Foundation for Civil Society, John Ulanga.

 Baadhi ya watoa mada katika semna hiyo, wakisikiliza michango iliyokuwa ikitolewa na washiriki wa semina hiyo, jijini jioni hii.

No comments:

Post a Comment