TANGAZO


Wednesday, June 13, 2012

UN yahamasisha Watanzania kujitolea damu

Bango lenye tangazo la siku ya kampeni ya utoaji damu, likiwa limewekwa barabarani kwa ajili ya kuhamasisha utoaji wa damu kwa kila mtu nchini katika maadhimisho ya Siku ya Kampeni ya Utoaji damu duniani.
  
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania Dk. Alberic Kacou, akiongoza wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa kujitolea damu ikiwa ni katika kuadhimisha Wiki ya Kampeni ya Kitaifa ya kujitolea damu nchini. Kulia ni Afisa Mtaalam wa damu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Deochris Kaimukilwa.


Dk. Alberic Kacou, akizungumza na waandsihi wa habari, jijini Dar es Salaam leo, mara baada ya kumaliza zoezi la kujitolea damu, ambapo amezungumzia changamoto za Umoja wa Mataifa unazokabiliana nazo katika kufanikisha zoezi la kuhamasisha watu kujitolea damu,  alizozitaja kuwa moja wapo ni ugumu uliopo katika kuwashawishi watu kujitolea kutokana na fikra za watu walizonazo kuhusiana na kujitolea damu.


Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Hoyce Temu akifanyiwa vipimo vya awali kabla ya kuchangia damu na Mtaalamu kutoka mpango wa Taifa wa Damu Salama, Edith Senga.



Mtaalamu kutoka mpango wa Taifa wa Damu Salama, Edith Senga, akitoa tathmini kwa waandishi wa habari kuhusiana na zoezi zima la utoaji damu linavyoendelea nchini katika maadhimisho hayo. (Picha zote na mdau wetu)

No comments:

Post a Comment